Dk Rose Migiro Awataka Wananchi Kuisoma Katiba Inayopendekezwa

Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro (katikati), akikata utepe kuzindua zahanati kwa  ajili ya matibabu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA Nakayama iliyopo katika Kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati mahafali ya pili yaliyofanyika Octoba 27,2014 (kulia), Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, na kushoto ni Kaimu Balozi wa Japan  nchini, Kazuyoshi  Matsu.

Baadhi ya wahitimu wa elimu ya sekondari  ya kidato cha nne kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakiwa wamejipanga tayari kuelekea sehemu maalumu iliondaliwa kwa ajili ya kuagwa.

Baadhi ya Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakifuatilia matukio.

Baadhi ya Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakifuatilia matukio.

Na Magreth Kinabo, MAELEZO

WANANCHI wameshauriwa kuisoma Katiba Mpya nayopendekezwa sura kwa sura na ibara baada ya ibara ili waielewe juu ya ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya Katiba na kuacha kusikiliza maneno ya watu pekee.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha Rose Migiro wakati wa sherehe za mahafali ya pili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA NAKAYAMA , iliyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Dk. Migiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi, wakiwemo baadhi ya wake za viongozi na wageni i wengine mbalimbali.

“Nchi yetu ilikuwa katika mchakato wa unadikaji wa Katiba Inayopendekezwa kazi ambayo ilikamilika Oktoba 8, mwaka huu. Kazi iliyombele yenu ni kuisoma Katiba hii sura kwa sura ibara kwa ibara. Tusikubali kusomewa na tutakapokamilisha kazi ya kuisoma tuipigie kura ya ndiyo,” alisema Dk. Migiro.

Akizungumza hivi karibuni katika mkutano wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China uliofanyika kwenye Nyumba ya kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai, Beijing, Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete alisema Kura ya Maoni inatarajiwa kupigwa wakati wowotemwezi Aprili 2015 kama mambo yataenda kama yalivyopangwa.

Wakati huo huo; Ubalozi wa Japan kupitia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje umetoa kiasi cha fedha cha sh. milioni 800, ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani 500,000 kwa ajili ya kuisaidia Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA Nakayama, iliyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Balozi wa Japan chini, Kazuyoshi Matsu naga wakati wa sherehe za mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika jana na kuhudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha Rose Migiro ambaye alikuwa mgeni rasmi baadhi ya viongozi, wakiwemo baadhi ya wake za viongozi na wagemi wengine mbalimbali.

“Juzi Idara ya Mambo ya nje ya Japan imekubali kutoa Dola za Marekani 500,000 kwa ajili ya mradi wa mpya wa awamu ya pili wa kusaidia shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama,” alisema Kaimu Balozi huyo.

Matsu naga aliongeza kwamba fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kompyuta na utawala, yakiwemo mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

“Sisi Wajapan tunapenda kuendelea kutoa msaada kadri inavyowezekana. Msaada wa leo utaongeza urafiki kati nchi ya Japan na Tanzania,” alisisitiza. Kaimu Balozi huyo alimataka kila wanafunzi wa shule hiyo, kutoa mchango wake katika kuleta maendeleo ya jamii kwa kutumia mafunzo aliyoyapata.

Kwa upande wake, Dk. Migiro, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, aliwataka wadau mbalimbali kuendelea kumsaidia Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete katika kusaidia wanafunzi hao ili kupanua fursa za watoto wa kike kielimu.

“Nimegundua kuwa mtoto wa kike anakabiliwa na upungufu wa fursa si kitaaluma. Hivyo kuchangia shule hii kwa mtoto wa ni kujenga na kuihimarisha ya fursa yake yeye binafsi na familia kwa ujumla.
Dk. Migiro alifurahishwa uweleadi wa wanafunzi wa shule hiyo, yakiwemo mazingira bora, ambapo alisema shule hiyo inaviwango bora.