BOT Kuimarisha Mfumo wa Utoaji Taarifa za Uchumi na Fedha

Baadhi waandishi wa habari wa za Fedha na Uchumi waliohudhuria Semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania Wakimsikiliza Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Juma Reli (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo leo mjini Bagamoyo Mkoani Pwani.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Juma Reli (katikati mwenye suti nyeusi) akiwaeleza waandishi wa habari za Fedha na uchumi kuhusu majukumu ya benki hiyo mara baada ya kufungua rasmi Semina kwa waandishi hao iliyolenga kuwaongezea ujuzi na weledi katika kuripoti habari za fedha na Uchumi.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Juma Reli akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari za Fedha na Uchumi (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina hiyo mjini Bagamoyo, Mkoani Pwani, Kulia ni Mwenyekiti wa washiriki hao Bw. Thomas Chilala na Kushoto ni Meneja Uhusiano na Itifaki wa Benki Hiyo Bi Zalia Mbeo.

Frank Mvungi- Maelezo, Bagamoyo

SERIKALI ya Tanzania imeahidi kuendelea kuimarisha mfumo wa utoaji taarifa za Uchumi na fedha kwa wananchi ili kuongeza wigo wa wananchi kushiriki katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo endelevu. Hayo yamesemwa leo mjini Bagamoyo na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Juma Reli wakati akifungua Semina kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha iliyoandalliwa na Benki hiyo.

Akifafanua, Reli amesema waandishi wa habari wanalo jukumu la msingi la kuuhabarisha umma kuhusu majukumu ya Benki hiyo katika kukuza uchumi na fursa zinazotolewa na Serikali ili kuwanufaisha wananchi.

“Navipongeza Vyombo vya habari hapa nchini kwa kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za uchumi na fedha kwa wananchi” alisema Reli.

Akizungumzia Lengo la Semina hiyo Reli amesema imelenga kuwaongezea ujuzi na weledi waandishi hao ili kuwasaidia wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo na namna wanavyoweza kunufaika nazo.

Naye Meneja Uhusiano na Itifaki wa BOT, Bi. Zalia Mbeo alisema kuwa mwaka huu waandishi wa habari wapatao 20 wanashiriki katika Semina hiyo ambapo mwaka jana ilifanyika kwa mara ya kwanza na ilihusisha waandishi wa habari 15.

Pia bi Mbeo alisema BOT itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari hapa nchini kwa kuwa ni wadau muhimu katika kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu Kazi zinazotekelezwa na Benki hiyo kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake.

Mada zitakazotolewa katika Semina hiyo ni pamoja na Ushiriki wa wananchi katika dhamana za Serikali, Soko la pamoja kwa nchi za Jumuiya Afrika Mashariki, Kurugenzi ya uchumi na Sera, Kurugenzi ya huduma za Kibenki na Sarafu, Kurugenzi ya usimamizi wa Mabenki, Kurugenzi ya Mifumo ya malipo na Bodi ya Bima ya Amana.