Rais Kikwete, Dk. Bilal wamuaga Jenerali Mayunga


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete na Makamu wake Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Mawaziri wastaafu, Joseph Sinde Warioba na Salim Ahmed Sailm, wakiwa katika shughuli ya mazishi kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayungi kwenye Viwanja vya Kambi ya Jeshi Lugalo leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Peter Mayunga, wakati wa shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha Luteni Jenerali mstaafu, Silas Peter Mayunga, aliyefariki hivi karibuni. Shughuli ya kuagwa kwa mwili wa marehemu Mayunga imefanyika leo, katika Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.


Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayungi, wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Viongozi wa Serikali, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, akitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Peter Mayunga, wakati wa shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR).