Mkenya Atolewa Jumba la Big Brother

Sabina Anyango

Sabina Anyango

MWAKILISHI wa Kenya ndani ya jumba la Big Brother, Sabina Anyango ametolewa ndani ya jumba hilo. Sabina ambaye ni mama wa mtoto wa miezi minane na ndio mkenya wa kwanza kufungishwa virago. Inadaiwa kuwa watazamaji na mashabiki wa shindano hilo waliamua kumpigia kura za kumtoa Sabina ili aende kumuhudumia mwanawe.

Ikiwa ni siku 14 pekee zilizopita mshiriki Sabina ameonekana kumkumbuka sana mwanawe ndani ya jumba hilo huku akionekana wakati mwingi akifunga vitu kwenye mgongo wake akiashiria kuwa amembeba mwanaye.

Mshiriki huyo ambaye alikuwa kipenzi cha wengi ndani ya jengo hilo alionekana kuweka pamoja blanketi na nguo na kuvifunga kwenye mgongo wake akiwa na kofia ya mwanaye huku akitembea katika nyumba hiyo kabla ya kujiunga na wenzake waliokuwa wakijivinjari nje.

Baadhi wanasema kufunga vitu mgongoni ndio chanzo za mashabiki kuanza kuomuonea huruma Sabina wakisema bora aende nyumbani kwa mwanawe mwenye miezi minane. Na hapo ndipo walipompigia kura Jumapili na kumtimua kutoka katika Big Brother house.

Sabina alitimuliwa kutoka katika nyumba hiyo pamoja na Lilian kutoka Nigeria na Esther wa Uganda. Hatua ya kumondoa Sabina katika Big Brother house inamwacha mwakili mmoj tu wa Kenya Melvin Alusa ambaye ni kakake Ben aime Baraza wa kikundi cha wanamuziki cha Sauti Sol.

-BBC