Rais Kikwete Ahitimisha Mafunzo ya Wakongo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe hizo Mkoani Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe hizo Mkoani Arusha.


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ametunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa Kitanzania 23 miongoni mwa maofisa 437 wa kundi la 53/13 – Kongo. Kundi hilo liliwajumuisha maofisa wa Kitanzania wapatao 23 na wahitimu 414 kutoka Kongo.

Jumla ya wanajeshi 414 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamehitimu mafunzo ya Uafisa katika chuo cha maafisa (TMA) Monduli baada ya kufanya kozi kwa muda wa mwaka mmoja. Maafisa hao wanafunzi kutoka Kongo walipata mafunzo hayo pamoja na maafisa watanzania 23 waliohitimu leo na kupata kamisheni ya cheo cha luteni usu baada ya kula kuapa mbele ya Mhe. Rais Dkt Jakaya Kikwete.

Tofauti na kamisheni zingine kwani pamoja na Mhe. Rais Kikwete aliweza kutoa Kamisheni kwa maafisa wapya wapatao 23 .
Aidha, kitu ambacho ni kigeni vijana kutoka kongo walihitimu pasi kutunukiwa kamisheni kwani kulingana na taratibu maafisa wa kongo wanapaswa kupewa kamisheni na Rais na wakiwa katika ardhi yao, hivyo wahitimu hao watakapewa kamisheni nchini mwao.

Akitoa shukurani kwa Rais Kikwete wa Tanzania, Rais Joseph Kabila ambaye alishuhudia maafisa wake wakihitimu mafunzo hayo, alisema anawashukuru kwa kukubali kutoa mafunzo kwa maafisa hao. Pia alisema anaamini atakuwa amepata makamanda wazuri watakaosaidia kuimarisha usalama nchini mwao na pia kuondoa maadui wanaohatarisha amani nchini Kongo.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria sherehe hizo Wazri wa Ulinzi na JKT, Mhe. Dkt Hussein Ali Mwimnyi, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, Katibu mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Waziri Mkuu Mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowasa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Magesa Mlongo, majenerali, majenerali wastaafu, na mabalozi wa kijeshi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

kwa upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Ulinzi, Alexander Luba Ntambo, na Waziri wa Mambo ya Nje, Raymond Tshibanda N’tungamulongo, Balozi wa Kongo nchini Jean Pierre Juma Alfani, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama Kahimbi Delphin na Mkuu wa Mafunzo, ya Kijeshi, brigedia Jenerali Aguru Mamba Maurice.