Biswalo Mganga Mkurugenzi Mpya wa Mashitaka

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete


RAIS wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.
Kabla ya uteuzi wake, Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.