Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umechangia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Msaada huo utatumika kununulia vifaa kwa ajili ya chumba cha Wagonjwa mahututi (ICU).
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili
Dk. Marina Njelekela aliishukuru NSSF kwa msaada huo na kuongeza kuwa msaada huo utaenda kuokoa maisha ya watanzania wengi.
Pia aliwashauri NSSF kushiriki kwenye clinic Maalumu ya upimaji wa Kansa ya Matiti kwa kina mama ambalo hufanyika hospitalini hapo. Naye Mwakilishi wa NSSF, Jumanne Mbepo alisema kua mchango uliotolewa na NSSF kwa hospitali hiyo hautoshi kununua vifaa vyote na kuomba Taasisi nyingine ziichangie Hospitali hiyo ili kuweza kuokoa maisha ya Watanzania wengi zaidi.
NSSF imekuwa ikitoa huduma ya bima ya Afya kwa wanachama wake ijulikanayo kama SHIB, Hospitali ya muhimbili ni mojawapo ya watoa huduma wa bima hiyo.