IDHAA ya Habari ya BBC (Panorama) imegundua kambi ya mateso inayosimamiwa na Majeshi ya Usalama nchini Zimbabwe, iliyopo katika eneo lenye utajiri wa madini ya almasi, mjini Marange.
BBC ilifanikiwa kuzungumza na walioathirika siku za karibuni ambao walielezea walivyopigwa sana na kudhalilishwa kijinsia.
Madai hayo yanatolewa huku Umoja wa Ulaya EU ukishinikiza kuruhusu baadhi ya almasi zilizopigwa marufuku kutoka nchi hiyo inayoongozwa na Rais Robert Mugabe kurejeshwa kwenye masoko ya dunia. Hata hivyo, Serikali ya Zimbabwe haijasema lolote kuhusu utafiti huo wa BBC.
Katika nyaraka iliyoonekana na BBC, EU ulisema kuwa sasa una imani kuwa migodo miwili eneo hilo zinafikia viwango vya kimataifa na kutaka almasi zinazoztoka eneo hilo kuidhinishwa haraka iwezekanavyo ili ziuzwe nje, ambayo itaondoa kizuizi cha biashara kilichowekwa mwaka 2009.
Kuzuiwa huko kuliwekwa na Kimberly Process (KP), shirika la kimataifa linalosimamia almasi, kufuatia ripoti za mauaji ya watu chungu nzima na udhalilishaji unaofanywa na majeshi ya usalama ya Zimbabwe katika eneo la machimbo la almasi huko Marange.
-BBC