Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akipokea dola elfu moja kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benk ya CRDB, Tully Esther Mwampamba akikabidhi mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Kiinjili Moroviani Tanzania (KKMT) Mburahati jijini Dar es salaam, kulia ni Askofu David Martin Mwalyambile wa kanisa hilo. Mama Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ambapo ziliweza kupatikana jumla ya milioni 128.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akimshukuru mtoto Cecylia Mashaka Mwaisaka mwenye umri wa miaka mitatu kwa kuchangia shilingi elfu ishirini kama mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Moroviani Mburahati jijini Dar es Salaam, Mama Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ambapo ziliweza kupatikana kiasi cha shilingi 128.
Kwaya ya Kanisa la Moroviani Mburahati ikitumbuiza katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa Kanisa lao. Shughuli hiyo ilifanyika Jumapili Septemba 29. Picha zote na Chris Mfinanga.
Picha za kumbukumbu shughuli za kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili Moroviani Tanzania (KKMT) Mburahati jijini Dar es salaam. Shughuli hiyo ilifanyika Jumapili Septemba 29. Picha zote na Chris Mfinanga.