Rasimu Katiba Inayopendekezwa Yawasilishwa Bungeni Leo

Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge

Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

RASIMU ya Katiba inayopendekezwa imewasilisha leo katika Bunge Maalum la Katiba mara baada ya Kamati ya Uandishi wa Katiba hiyo kumaliza kazi ya kuiandaa iliyopewa na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Akiwasilisha Rasimu hiyo ya Katiba inayopendekezwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge alisema katika mchakato wa kuandika katiba hiyo kamati yake imezingatia mishingi mitatu; yaani maoni ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba toka katika Kamati 12 kama zilivyowasilisha, Katiba za nchi nyingine duniani pamoja na taratibu za uandishi wa katiba kikawaida.

Akifafanua alisema rasimu hiyo kimuundo itakuwa na Serikali mbili, pamoja na viongozi wa ngazi za juu watatu; yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wake pia na Makamu marais wengine wawili. Alisema Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziber (SMZ) pamoja na Waziri Mkuu watakuwa ni Makamu wa Rais mbali ya nyazifa zao.

Kwa msingi huo Chenge alisema kutakuwa na makamu marais watatu yaani yule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Rais wa SMZ na Waziri Mkuu wa Tanzania. Kuwasilishwa kwa rasimu hiyo kunatoa nafasi sasa kwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kujiandaa na zoezi la upigaji kura uliopangwa kufanyika Septemba 29 hadi 2 Oktoba mwaka 2014.

Taarifa zaidi juu ta Rasimu hiyo ya Katiba iliyopendekezwa baadaye kidogo. Baki nasi…!