RC Awatahadharisha NIDA Juu ya Wahamiaji Haramu

Mkurugenzi Mifumo ya Komputa NIDA, Joseph Makani akizungumza.

Mkurugenzi Mifumo ya Komputa NIDA, Joseph Makani akizungumza.


Na Yohane Gervas, Rombo
KUFUATIA uwepo wa wimbi kubwa la wahamiaji haramu mkoani Kilimanjaro, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini (NIDA) imetakiwa kuwa makini katika zoezi la utambuzi na usajili wa watu mkoani humo kabla ya kutoa vitambulisho.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya Moshi, Dk. Ibrahim Msengi, wakati akisoma taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidasi Gama katika semina ya utoaji wa elimu kuhusu utambuzi na usajili wa watu mkoani hapa.

Gama alisema kutokana na Mkoa wa Kilimanjaro kuwa changamoto kubwa ya muingiliano wa watu kutoka mataifa mbalimbali na kwamba ni vyema NIDA ikwafanya kazi kwa kushirikiana na uhamiaji ili kuweza kufanya kazi hiyo kwa ufasahaa.

“Watendaji wa NIDA ni vizuri sasa mkawa makini katika uendeleshaji wa zoezi ambalo linaenda kufanyika mkoani hapa kwani kunachangamoto kubwa ya wahamiaji haramu kutokana na eneo letu lipo mpakani sasa nawatakeni mfanya kazi kwa uadilifu na uaminifu,” alisema Gama

Aidha Alisemakuwa kutokana na zoezi hilo kukamilika kwa baadhi ya mikoa wananchi wamekuwa wakipata usumbufu wa mara kwa mara jambo ambalo limekuwa likiwakatisha tamaa na kuacha kushiriki kujiandikisha, hivyo kuwataka NIDA kuainisha changamoto wanazokumbana nazo ili waweze kuzikabili.

“Ni vema watendaji hao wakakupunguza usumbufu kwa wananchi na kuwa elimisha juu ya umuhimu wa kushiriki katika zoezi hilo ili malengo yao mamlaka hiyo yaweze kufikiwa kwa urahisi,” alisema Gama.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka hiyo Severine Momburi, alisema wananchi kupata vitambulisho vya taifa watapata faida nyingi ambazo zitapunguza migogoro ya mara kwa mara ya wakulima na wafugaji kwa kuweka mgawanyiko mzuri wa matumizi ya ardhi. Alisema faida nyingine ni ile ya ugawaji wa pembezjeo za kilimo kwa wakulima na upangaji wa vipaumbele vya maendeleo katika mikoa ikiwa ni pamoja na kuinua pato la taifa na la mtu mmoja mmoja.

Alisema zoezi la utambuzi kwa Mkoa wa Kilimanjaro linatarajiwa kuanza Oktoba 11, 2014 na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu na kujitokeza kwa wingi na kwamba wanachi watapatiwa elimu sahihi kuhusu utaratibu wa utambuzi na usajili.