Msafiri Diof wa Twanga Pepeta Avunja Mayai Jukwaani

Msafiri Diof wa Twanga Pepeta akiimba jukwaani katika onesho hilo.

Msafiri Diof wa Twanga Pepeta akiimba jukwaani katika onesho hilo.

Hapa ndipo Msafiri Diof wa Twanga Pepeta alivunja moja ya yai kabla ya kuanza kuimba.

Hapa ndipo Msafiri Diof wa Twanga Pepeta alivunja moja ya yai kabla ya kuanza kuimba.

Msafiri Diof wa Twanga Pepeta kifanya mambo jukwaani.

Msafiri Diof wa Twanga Pepeta kifanya mambo jukwaani.

Kiongozi Luiza Mbutu wa Twanga akiwajibika jukwaani katika onesho hilo.

Kiongozi Luiza Mbutu wa Twanga akiwajibika jukwaani katika onesho hilo.

RAPA nyota na mwimbaji wa muziki wa dansi, Msafiri Diof ambaye kwa sasa amerudi katika Bendi ya Twanga Pepeta juzi aliwashangaza mashabiki wa bendi hiyo baada kupanda jukwaani na kuvunja mayai mawili mbele ya jukwaa akidai ni ishara ya kujikinga na nuksi zozote baada ya kurejea tena kwenye bendi hiyo.

Diof alifanya vituko hivyo juzi wakati akitambulishwa rasmi na bendi hiyo kwa mashabiki wa Tabata katika onesho lililofanyika kwenye ukumbi wa Da’ West Park uliopo eneo la Tabata jijini Dar es Salaam. Rapa huyo mkongwe ambaye aliwahi kuvuma kipindi cha nyuma akiwa na bendi hiyo aliwashangaza mashabiki baada ya kupanda jukwaani kabla ya kuanza kuimba alitoa mayai mawili aliyokuwa nayo mfukoni na kuyapasulia chini upande wa kushoto na kulia wa jukwaa. “…Tunafanya hivi ili kuondoa mikosi kwa wale wote wasiotutakia heri na pia kuonesha nimerudi,” alisema Diof huku akivunja mayai hayo.

Diof ambaye alionekana kushangiliwa na wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo, mara baada ya kupanda jukwaani ghafla na kuanza kuimba, pia alisema kwa sasa amerudi kivingine huku akiwa na staili mpya ya kugani ambayo anaamini itakuwa na mvuto kwa mashabiki wanaoisapoti bendi yao. Akizungumza mashabiki kiongozi wa Bendi hiyo, Luiza Mbutu alisema bendi hiyo imeongeza nguvu kazi ya bendi kwa kuleta waimbaji, marapa na wanenguaji wapya ili kuleta mvuto zaidi kwa wapenzi wake.