Bara la Afrika Linaweza Kuondoa Umaskini – Rais Kikwete

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi ya ngao na kikombe toka kwa  mwakilishi wa CCM New York na Vitongoji vyake, Isaack Kibodya kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington. Kombe hilo ni la pongezi kwa ulezi wake katika michezo na sanaa nchini Tanzania.

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi ya ngao na kikombe toka kwa  mwakilishi wa CCM New York na Vitongoji vyake, Isaack Kibodya kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington. Kombe hilo ni la pongezi kwa ulezi wake katika michezo na sanaa nchini Tanzania.

Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane aliejitambulisha kwa jina la Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Dkt Seche Malecela baada ya kupokea risala ya pongezi kwa uongozi wake nchini Tanzania  katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea makombe toka kwa Balozi wa Heshima wa Tanzania huko California Mhe Ahmed Issa kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka Watanzania kutoka Atlanta  kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka Watanzania kutoka Atlanta  kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi ya ngao na kikombe toka kwa  mwakilishi wa  CCM New York na Vitongoji vyake  Bw. Isaack Kibodya  kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington. Kombe hilo ni la pongezi kwa ulezi wake katika michezo na sanaa nchini Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington.
Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi.

Bara la Afrika Linaweza Kuondoa Umaskini – Rais Kikwete

PAMOJA na changamoto nyingi ambazo nchi za Afrika zinakumbana nazo, bado kuna uwezekano wa kuondosha umaskini katika bara hilo. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jana  tarehe 19 Septemba, 2014 jijini Washington DC katika hotuba yake kwenye mkutano unaojadili  Maendeleo na  kumaliza Umaskini,  mkutano uliondaliwa  na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

” Tukiwa  na  sera sahihi, Serikali kuingilia kati pamoja na ushirikiano  na sekta binafsi, inawezekana kuondoa umaskini. Juhudi hizi zikifanikiwa inawezekana kuondosha kabisa umaskini” Rais amesema.

Mkutano wa USAID Frontiers in Development, Ending Extreme Poverty, pia umehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bw. John Kerry ambaye katika hotuba yake ya ufunguzi, amemzungumzia Rais Kikwete kuwa ni kiongozi mtendaji na ambaye amechangia katika kuleta Amani katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu na kukuza utawala Bora nchini Tanzania.

“Maneno ya Rais Kikwete, sio maneno tu, ni kiongozi anayetenda na kufanikisha mambo, tunamshukuru kwa kukuza Amani katika nchi za Maziwa Makuu na utawala Bora Tanzania,” Amesema Bw. Kerry.

Akitolea mfano wa mafanikio ambayo Tanzania imeyafikia hadi sasa katika mkutano huo, Rais Kikwete ameelezea hatua za maendeleo na kiuchumi  pamoja na changamoto zake kuanzia wakati wa Uhuru hadi leo. Amesema mafanikio ya kiuchumi yameanza kuonekana nchini Tanzania baada ya kutangazwa kwa Mageuzi ya Kiuchumi kwenye miaka ya 1980 ambapo nchi imedumu nayo na kuonyesha mafanikio.

“Uchumi umekua kutoka asilimia 3.5 Mwaka 1990 hadi kufikia  kiwango cha asilimia 7 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita”

Rais Kikwete amewaeleza washiriki mbalimbali na wageni waalikwa na kuelezea waziwazi kuwa pamoja na mafanikio hayo, bado kiwango cha kuondosha umaskini hakijaridhisha vya kutosha.

Rais ameelezea kuwa kiwango hiki cha uchumi hakiridhishi kwa sababu sekta muhimu ya kilimo ambayo ndiyo inayotoa ajira kwa Watanzania wengi, haijakua na kuendelea vya kutosha na badala yake sekta zinazohusika na utoaji huduma, mawasiliano, ujenzi, uzalishaji na madini ndiyo zimekua zaidi.

“Sekta ya kilimo ambayo ndiyo inawahudumia Watanzania wapatao asilimia 75 kwa njia ya ajira na kujikimu kimaisha imekua kwa wastani wa asilimia 4.2 katika kipindi cha miaka 10”

Amesema na kuainisha kuwa tatizo hili ndilo limefanya juhudi za kuondosha umaskini nchini Tanzania kutokufanikiwa kwa kiwango kinachotarajiwa.

Rais Kikwete yuko nchini Marekani, kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumatano tarehe 24 Septemba, 2014.

Pamoja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Kikwete anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani, mkutano ambao unatarajiwa kuwa nchi za Afrika zitatoka na msimamo wake kuhusu suala la Mabadiliko ya Tabia Nchi, msimamo ambao utajadiliwa na kupelekwa katika Umoja wa Mataifa katika kikao chake kikubwa kuhusu Tabia nchi kinachotarajiwa kufanyika tarehe 23 Septemba, 2014.