Hatuna Tofauti ya Mpaka Kati ya Tanzania na Malawi – Waziri Malawi

Waziri wa Habari , Utalii na Utamaduni Nchini Malawi  Kondwani Nankumwa akizungumza na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya Ofisini kwake.

Waziri wa Habari , Utalii na Utamaduni Nchini Malawi, Kondwani Nankumwa akizungumza na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya Ofisini kwake.

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi  Patrick Tsere Akizungumza na waandishi wa Habari kutoka Mbeya walipotembelea Ofisi za ubalozi Nchini Malawi.
Baadhi ya Waandishi wakimsikiliza Balozi.

 Balozi wa Tanzania Nchini Malawi  Patrick Tsere akijibu Taarifa ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya .

 Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni, Kondwani Nankumwa

 Wa kwanza Kulia ni Ofisa Habari wa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni akifuatilia Mkutano huo

Francis Phiri wa kwanza kulia ambaye ni Mratibu wa ziara hiyo Nchini Malawi na Muasisi wa Nyika Press Club ya Malawi akiwa katika Mkutano huo.
Kikao kikiwa Kinaendelea 

Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Nchini Malawi   Kondwani Nankumwa wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Kutoka Mkoa wa Mbeya nje ya Ofisi yake Jijini Lilongwe.

WAZIRI wa Habari,Utalii na Utamaduni nchini Malawi  Kondwani Nankhumwa amesema kuwa Serikali ya Malawi haina mgogoro na Serikali ya Tanzania kuhusiana na mpaka wa ziwa Nyasa.
 
Aliyasema hayo baada ya kukutana na Jopo la Waandishi Habari wa Mkoa wa Mbeya waliotembelea ofisini kwake katika mfululizo wa ziara ya waandishi waliofanya ziara ya juma moja nchini humo katika ziara ya kubadishana uzoefu baina ya Waandishi wa Nchi hizo.
 
Waziri Nankhumwa alisema kuwa Mtoto wa Rais  wa Malawi Profesa Ather Muthalikana anasoma Dar es Salaam naye Rais amekuwa Muhadhiri wa chuo kikuu na kwamba Watanzania wengi wanaishi na kufanya biashara nchini Malawi hivyo hakuna sababu za kuwepo kwa tofauti za aina  yoyote ile itayowapelekea kuwagawa wananchi wa pande hizo.
 
Aidha alisema kuwa ili kuonesha hakuna tofauti baina ya wananchi wa pande hizo Marais wa nchi hizo watapaswa kuchukua ndoano na kuvua samaki pamoja katika ziwa hilo ili kuionesha Dunia
kuwa wananchi wa pande hizo ni wamoja na kuna mwingiliano wa makabila.
 
Kauli hiyo iliungwa mkono na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere ambaye alisema kuwa hakuna mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Tanzania na Malawi.
 
Aliyasema hayo alipotembelewa na waandishi wa Habari wa Mkoa Mbeya walipotembelea ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi katika mfulizo wa ziara ya waandishi hao nchini Malawi ili kubadilishana mawazo na changamoto mbalimbali zikiwemo za mazingira, utalii na Elimu juu ya Ukimwi ambazo zinafanana katika nchi hizo.
 
Balozi Tsere alisema hivi sasa si wakati wa marumbano kwani inahitajika subira katika mzungumzo yaliyonza baina ya viongozi wa nchi hizo na kwamba si wakati wa kuupeleka mgogoro huo katika mahakama ya  kimataifa ambapo utazigharimu fedha nyingi nchi hizo katika utatuzi wa mgogro huo.
 
Hata hivyo Waandi wa Habari wa nchi hizo walifanya makubaliano ambayo yatasaidia kuzitangaza nchi hizo kimataifa ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama zilizopo Malawi na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe ili utumiwe na wananchi hizo ili kukuza uchumi wan chi hizo.
 
 
Chanzo: Mbeya Yetu Blog, Lilongwe Malawi.