Yambeshi Awataka Watumishi wa Umma Mwanza Kuzingatia Sheria

KATIBU MKUU UTUMISHI GEORGE YAMBESHI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA RS MWANZA(PICHA NA AFISA HABARI WA RS MWANZA)

KATIBU MKUU UTUMISHI GEORGE YAMBESHI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA RS MWANZA(PICHA NA AFISA HABARI WA RS MWANZA)

KIKAO CHA KATIBU MKUU UTUMISHI NA WAFANYAKAZI KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA(PICHA ZOTE NA AFISA HABARI RS MWANZA.)

KIKAO CHA KATIBU MKUU UTUMISHI NA WAFANYAKAZI KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA(PICHA ZOTE NA AFISA HABARI RS MWANZA.)

KATIBU MKUU UTUMISHI GEORGE YAMBESHI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA..

KATIBU MKUU UTUMISHI GEORGE YAMBESHI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA..

Na Atley Kuni – Ofisa Habari Mwanza
 
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi George Yambeshi, amewataka watumishi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuleta tija katika ufanisi wa kazi zao.
 
Ameyasema hayo wakati alipokutana na watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mwanza hii leo alipokuwa ziarani mkoani humo kwa shughuli za kijamii na kuamua kutumia fursa hiyo kukutana na watumishi hao.
 
Yambeshi amesema kama watumishi wa umma ni lazima kuzingatia miiko inayo ongoza utumishi wa umma huku akitolea mfano wa mavazi nadhifu kwa watumishi na yasiyo na utata kwa watu. “Kama watumishi wa ni vema kuzingatia miiko inayo tuongoza” alisema na kuongeza. kuwa suala la kuvujisha siri za serikali ni suala lisilo kubalika hivyo moja ya sifa ya mtumishi wa umma ni lazima ajue kutunza siri.
 
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo ameonya watumishi wa kuacha kuchanganya mambo ya siasa mahali pa kazi” Ndugu zangu haikazwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa lakini sio vema mtumishi kufanya masuala ya siasa mahali pa kazi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
 
Mbali na masuala la siasa na uadilifu katika kazi, pia katibu Mkuu huyo ametumia fursa hiyo, kusilikiliza kero mbalimbali za watumishi hao ikiwapo suala la kodi kubwa, mikopo kwa watumishi pamoja na kukosekana kwa baadhi ya miundo ya kada mpya za utumishi serikialini.
 
Awali akimkaribusha katibu Mkuu kiongozi kuzungumza na watumishi hao wa Skretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bwana Ndaro Kulwijila, alimuelezea kuhusu hali halisi ya watumishi katika mkoa wa Mwanza huku akitoa kilio chake kwa Katibu Mkuu huyu juu ya utofauti Mkubwa wa mishahara baina ya watumishi waliopo kwenye wakala wa serikali na wale wa serikali kuu.
 
Hata hivyo katika majibu yake Katibu Mkuu huyo aliahidi kushughulikia changamoto zote zilizo jitokeza katika kikao hicho na kuzipatia ufumbuzi kwa kadri itakavyowezekana. Katibu Mkuu Utumishi ndiye mkuu wa masuala ya Utumishi wa umma katika Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.