Magonjwa ya Moyo Bado Yachangia Vifo Vingi Tanzania

Ahmedabad Apollo Hospital.

Ahmedabad Apollo Hospital.

KWA mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zilizotolewa mwaka 2011, Vifo vilivyotokana na magojwa ya moyo nchini Tanzania vilifikia idadi ya watu 19,083, au asilimia 4.33% ya idadi ya vifo vyote.
Na takwimu hizo zilionesha idadi ya wanaofariki ni watu 117.64 kati ya watu 100,000, huku takwimu hizi zikiiweka Tanzania katika nafasi ya 87 ulimwenguni.
Magonjwa haya ya moyo yanasababisha vifo vipatavyo idadi ya watu milioni 12 kwa mwaka duniani kote. Hata hivyo shirika la Afya Duniani limekua likifanya jitihada za lazima za kujaribu kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo na sababu zinazochangia kuongezeka kwa vifo hivyo. Magojwa haya ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kiharusi, shinikizo la damu, ugonjwa wa pembeni wa mishipa ya moyo, ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa na moyo kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

Katika kuonyesha kukua kwa maendeleo ya kiteknolojia ya huduma za afya, Hospitaliya Apollo ya mjini Gujarat, katika Mji wa Ahmedabad, ilifanikiwa kufanya upasuaji unaojulikana kitaalam kama ‘Bentall Surgery’ kwa mwanamke aliyekuwa na zaidi ya miaka 50. Upasuaji wa aina hii mara nyingi ni adimu kufanyika katika nchi ambazo ni masikini na zenye wataalamu wachache, ama zenye mfumo wa chini wa huduma za afya. Upasuaji huu uliofanywa kwa mwanamama kutoka Tanzania, ulikuwa ni wa aina yake, na ulichukua muda wa saa saba. Hii inaonyesha jinsi gani hospitali hizi zilivyo na uwezo na utaalam wa hali ya juu.

Mama huyo alikuwa akilalamika toka mwaka 2009 kuhusu maumivu ya mgongo, na alipofanyiwa uchunguzi wa kina, ilionekana kuwa alikua na matatizo katika moyo wake, ambayo hata hivyo hayangeweza kutibiwa hapa nchini. Alipelekwa katika hospitali ya Apollo ya mjini Ahmedabad, hospitali inayosifika kwa kufanya upasuaji kwa ufasaha na uhakika zaidi.
Mama huyu alifanikiwa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa moyo uliochukua zaidi ya masaa saba, ilionekana kuwa alikua na matatizo makubwa katika mishipa ya Aorta ambayo ilisababisha moyo wake ushindwe kufanya kazi kama kawaida. Hatimaye upasuaji huo ulifanikiwa, na pengine asingeweza kupona kama bado angelikuwapo nchini hapa, na hali yake inaendelea vizuri.

“…Katika masuala ya afya, Bara la Afrika liko kama Bara la Asia miaka 25 ama 30 iliyopita. Wale tu wenye kipato cha juu ndiyo wanaoweza kumudu huduma za uhakika nje ya nchi’’, Anasema Dr Hari Prasad, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali za Apollo.
“Ni wakati muafaka sasa wa kutumia uwezo wetu na utaalam wetu kuwatibu wenye matatizo. Tulichoifanyia India hatunabudi kuifanyia dunia nanchizinazoendelea, Anaongezea Dk. Pratap C Reddy, Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo
Mbali na Tanzania, Hospitali ya Apollo imepania kukita mizizi yake katika nchi mbalimbali za Afrika, ambako imekua ikipokea idadi ya wagonjwa wengi kutoka bara hili, na inamatarajio ya kuanzisha vituo kadhaa vya Afya katika eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika magharibi hapo mbeleni.
Zaidi kuhusu hospitali za Apollo;
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo “Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu”.

Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini India.