Daktari Mwingine Aambukizwa Ebola

Wahudumu wa Ebola wakivalishana mavazi maalumu kwa ajili ya kutoa huduma.

Wahudumu wa Ebola wakivalishana mavazi maalumu kwa ajili ya kutoa huduma.

DAKTARI, Olivette Buck ambaye alikuwa ni miongoni mwa madaktari wanaowatibu wagonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone ameguduliwa kuambukizwa ugonjwa huo baada ya kufanyiwa vipimo. Dk. Olivette Buck anakuwa ni daktari wa nne kukumbwa na ugonjwa huo kutoka nchi za Afrika Magharibi. Madaktari wengine watatu walioshikwa na ugonjwa huo tayari wamefariki dunia. Akizungumzia tukio hilo Waziri wa Afya wa Sierra Leone, Sidie Yahya Tunis amesema taratibu zinafanywa ili aweze kusafirishwa nchi za nchi kwa matibabu zaidi.

Janga hatari la ugonjwa huo wa Ebola limezikumba pia nchi za Liberia, Guinea, Nigeria pamoja na Senegal huku ikiarifiwa tayari zaidi ya watu 2,200. Ugonjwa wa Ebola unawaweka hatarini zaidi wahudumu wa waathirika kutokana na aina ya uambukizaji wake, kwani mtu anaambukizwa kwa kugusana na maji maji yoyote kutoka kwa mwili wa mgonjwa au maiti ya mgonjwa.

Kutokana na aina hiyo ya uambukizaji tayari wahudumu 135 wamepoteza maisha baada ya kujikuta wanaambukizwa wakiwa kazini. Idadi ya wafanyakazi na wahudumu wa afya waliokufa wamezidisha uhaba wa wauguzi na wafanyakazi wengine. Waziri wa Mawasiliano wa Liberia, Lewis Brown juzi aliwaeleza wanahabari kuwa hali katika nchi hiyo ni mbaya kutokana na ugonjwa huo, na sasa kwa mjini tu wanahitaji vitanda 1000 kwa ajili ya kutoa huduma kwa waathirika.

Aidha aliomba nchi hiyo kusaidiwa kwani kadri ya madhara yanavukuwa makubwa yanaenea na maeneo mengine. “…Hili ni janga la wote hivyo tunaitaji kusaidiwa maana madhara ya virusi hawa ni makubwa na yanaendelea kusambaa,” alisema Brown.

Ugonjwa huo hadi sasa umeathiri uchumi wa nchi ya Liberia kwa kiasi kikubwa hivyo kuna kila haja ya nchi kusaidiwa kurejesha hali ya uchumi sawa baada ya ugonjwa.

Umoja wa mataifa, UN umesema zaidi ya dola milioni 600 zinaitajika kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo wa hatari Ebola katika nchi za Afrika Magharibi na kuendelea kuhimiza misaada kutolewa. Tayari UN imetumia Dola milioni 100 kukabiliana na hatari hiyo.
-AP