Naibu Waziri wa Fedha alipotembelea Banda la Wizara hiyo Maonesho ya Nane Nane Dodoma


Naibu Waziri wa Fedha Pereira Silima (kulia) alipata maelezo jana juu ya mpango wa hiari kutoka kwa Ofisa Masoko Mwandamizi, James Mlowe (kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya wakulima ya Nane Nane ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma.


Naibu Waziri wa Fedha, Pereira Silima (kulia) akipata maelezo juu ya madeni ya ndani kutoka kwa Mhasibu aliyechini ya Idara ya Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha, Huruka Mwinyigogo (kushoto) alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho
ya wakulima ya Nane Nane ambayo yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma.


Ofisa Uhisiano Mwandamizi wa Chuo cha Mipango Dodoma, Godrick Ngoli (kushoto) akimweleza Naibu Waziri wa Fedha, Pereira Silima (kulia) juu ya mpango wa chuo wa kufungua tawi la Astashahada ya Mipango vijijini mjini Mwanza ili kuongeza idadi ya wananfunzi wakati alipotembelea maonesho hayo mjini Dodoma.


Mchumi kutoka Idara ya Bajeti ya Serikali , Wizara ya Fedha, Adamu Msumule (kushoto) akimweleza Naibu Waziri wa Fedha Pereira Silima (kulia) jinsi wanavyowaelimisha wananchi juu ya mchakato wa maandalizi ya bajeti ya Serikali kabla ya kuwalishwa Bungeni.


Mchambuzi wa Hesabu za Fedha kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Joseph Uiso (kushoto) akimweleza Naibu Waziri, Pereira Silima (kulia) jinsi CMSA inavyowaelimisha wananchi kupambana na upatu haramu nchini wakati alipotembelea maonesho hayo leo hii mjini Dodoma. Picha zote na Vicent Tiganya, MAELEZO-Dodoma.