DC Mushi Azinduwa Kampeni ya Kusafisha Jiji la Dar

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd. wadau na wananchi wakijipanga tayari kuanza kampeni ya wiki tatu ya kusafisha maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji iliyozinduliwa rasmi na Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi ikiwa ni awamu ya kwanza kwa mwaka huu kabla ya kuelekea kwenye kata nyingine mbili zilimo ndani ya manispaa ya Ilala wakishirikiana na wananchi.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd. wadau na wananchi wakijipanga tayari kuanza kampeni ya wiki tatu ya kusafisha maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji iliyozinduliwa rasmi na Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi ikiwa ni awamu ya kwanza kwa mwaka huu kabla ya kuelekea kwenye kata nyingine mbili zilimo ndani ya manispaa ya Ilala wakishirikiana na wananchi.

DSC_0423

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari na wananchi wa Kata ya Kisutu muda mfupi kabla ya kuzindua kampeni ya chukia uchafu katika kata tatu za wilaya hiyo. Kata hizo ni Kisutu, Mchafukoge na Kivukoni. Kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Kheri Kessy na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo.

DSC_0496

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (aliyebeba jiwe) akishiriki zoezi hilo.

DSC_0442

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Kheri Kessy akizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa rai kwa wananchi wa kata hizo kuunga mkono kampeni hiyo yenye lengo la kung’arisha vitongoji vya manispaa ya Ilala na wengine waige kutoka kwao.

Na Mwandishi Wetu

WILAYA ya Ilala imeanzisha kampeni ya wiki tatu ya usafi  katika maeneo yaliyopo katikati ya Jijini la Dar es Salaam kwa lengo la kutoa elimu na kuyaweka maeneo hayo safi na salama. Kampeni hiyo ilizinduliwa mwishoni mwa juma katika eneo la Kisutu na Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi.

Akizundua kampeni hiyo alisema bila suala la usafi kufanyiwa kazi, wageni wataona kwamba mambo katika Jiji la Dar e s Salaam ni hovyo hasa ikizingatiwa kwamba kati ya jiji ndio sebule ya Jiji. Kampeni hiyo inayosimamiwa na kampuni yenye dhamana ya usafi katika eneo hilo la kati ya Green Waste Pro Limited inashirikisha wananchi kwa lengo la kuwafanya wawe washirika wa usafi kwa kujenga utamaduni wa kuchukia uchafu.

Mkuu huyo wa wilaya pamoja na kushukuru wananchi na wanafunzi wa shule ya Kisutu waliofika  katika kampeni aliwataka viongozi kujipanga kuhakikisha kampeni hiyo inakuwa endelevu na yenye mafanikio. Kampeni hiyo inafanyika katika kata ya Kivukoni, Kisutu na Mchafukoge.

Pamoja na Mkuu huyo wa wilaya kusema kwamba kampeni hiyo ni chachu kwa kata za pembezoni za kujali  usafi amewataka wananchi kuwa washiriki kw akuhakikisha hawatupi uchafu hovyo. Naye Naibu Meya na Diwani wa Kisutu Kheri Kessy alisema kazi ya usafi inakabiliwa na changamoto kubwa hasa kutokana na kuvuja kwa chemba za maji machafu na wananchi kutupa taka hovyo.

Alisema wananchi  na hasa wapiti njia kama wakijifunza kutupa uchafu maeneo wanayotakiwa watakuwa wamesaidia sana kujenga utamaduni wa kuchukia uchafu na pia kufanya maeneo yapendeze. Alisema wananchi wa kata yake ya Kisutu ni waelewa tangu kuanza kwa kampeni hizo miaka miwili iliyopita lakini wapiti njia wamekuwa wakivuruga utaratibu wa usafi.

Aliwataka wakazi wa dare s salaam kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha hawatupi taka hovyo na kuanza kuuchukia uchafu kutoka katika majumba yao hadi wanakotembea.

Kampuni inayoendesha kampeni hiyo ya Green Wate kupitia kwa meneja wao Abdallah Mbena amesema kwamba kuna maendeleo makubwa katika kamepni za kuweka Jiji safi na safari hii wamewaalika wenzao kutoka Segerea na Upanga ili waone njia wanazotumia kuweka maeneo yao yenye dhamana safi na ya kupendeza.

Mbena alisema changamoto kubwa zinazokabili juhudi za kuweka maeneo safi ni upungufu wa usimamizi katika sheria kwani wengi hawakubali kuzitii. Alisema kama wangelizitii kungelikuwa na usafi kila siku. Kwani wengine wamekuwa wakifika katika majengo yao na kuyasafisha na kutupa uchafu barabrani wakati wafagiaji wameshafanyakazi yao usiku.

DSC_0469

Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.

DSC_0420

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya wasichana ya sekondari Kisutu  na wafanyakazi wa Green Waste Pro ltd. Waliojumuika na kampuni ya Green Waste Pro Ltd kuunga mkono kampeni hiyo iliyopewa jina na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ya “Chukia uchafu”.

DSC_0413

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo kwenye picha ya pamoja na watendaji wa manispaa ya Ilala na madiwani wa kata hizo tatu.

DSC_0493

Baadhi ya madiwani na wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd. wakimwaga taka kwenye gari maalum la kampuni hiyo kwenye maeneo ya katikati ya jiji wakati wa kampeni hiyo iliyoanza mwishoni mwa juma.

DSC_0511

Zoezi la usafi likiendelea ikiwemo kukusanya madumu ya maji pamoja na maboksi ya wauza matunda na mboga mboga yanayozagaa maeneo ya Kata ya Kisutu kama inavyoonekana pichani.