Mbunge Awataka Wananchi Kuacha Kilimo na Kufuga Nyuki

Mbunge wa Jimbo la Rombo (CHADEMA), Joseph Selasini

Mbunge wa Jimbo la Rombo (CHADEMA), Joseph Selasini


Na Yohane Gervas, Rombo
WANANCHI wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wametakiwa kupanda miti na kujishugulisha na ufugaji wa nyuki na kuacha kulalamikia wanyama pori aina ya nyani na temba wanaoharibu mazao ya mahindi.

Hayo yalisema jana na mbunge wa jimbo hilo Joseph Selasini, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ushiri wilayani humo, ambapo alisema ni vyema wananchi wakajishugulisha na ufugaji wa nyuki nakuacha kulalamikia wanyama pori ambao wamekuwa wakiharibu mazao.

Selasini alisema kumekuwapo na malalamiko mengi ya wananchi wanaozunguka hifadhi kulalamikia kuharibiwa mazo na wanyama pori hali ambayo inawarudisha nyuma kimaendeleo.
“Naona ni vyema wakulima waoteshe miti na kufuga nyuki ambapo watapata fedha nyingi kwa kuuza asali, na kuachana na kilimo cha mahindi ambayo yanaharibiwa na wanyama kama Tembo na Nyani ambao wamekuwa wakivamia mashamba kipindi cha mavuno,” alisema Selasini.

Alisema asali kwa sasa inauzwa kwa bei gali na kwamba lita moja ya asali ni silingi 36,000/ na kwamba ukiwa na mizinga mingi ya asali wafugaji hao watapata kipato kikubwa kuliko kulima kwa hasara na mazao hayo kuharibiwa na wanyamapori.

Aidha aliwataka wananchi wilayani humo kujitokeza na kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi bora na sio kiongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.

Alisema wananchi wakiweka viongozi bora katika ngazi za chini matatizo yao yatatatuliwa kirahisi kuliko kuweka viongozi ambao hawafai hali ambayo itawafanya kutotatuliwa kero mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo.