JK Awasili Kenya kwa Mkutano Maalum

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewasili Nairobi, Kenya, usiku wa Septemba Mosi, 2014, tayari kwa kuhudhuria Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi zinazounda Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) ambako Tanzania ni mwanachama.

Mkutano huo wa siku moja ambao utajadili ugaidi na athari zake kwa nchi za Afrika umepangwa kufanyika, Septemba 2, 2014 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki Moon.