Ujerumani Kusaidia Silaha Iraq, Marekani Waombwa Silaha

Baadhi ya silaha za jeshi la Ujerumani.

Baadhi ya silaha za jeshi la Ujerumani.

UJERUMANI inatarajia kupeleka silaha kwenye Jeshi la Wakurd wa Iraq zikiwemo bunduki na silaha nzito zinazoweza kutumika kushambulia kwenye vita kukabiliana na mashambulizi ya vifaru vya kivita. Jeshi hilo limekuwa likipambana na wapiganaji wa Kiislamu kaskazini mwa Iraq. Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Ursula Von der Leyen alisema silaha hizo zinauwezo wa kutumiwa na wanajeshi wapatao elfu nne ifikapo mwishoni mwa Septemba, 2014.

Alisema uamuzi huo ni kutokana na maslahi ya nchi yake. Hatua hiyo iliyochukuliwa na Ujerumani imeelezwa kuwa ni ya nadra sana kwa nchi hiyo, kupeleka silaha kwenye eneo lenye mapigano. Hata hivyo uamuzi huo umekosolewa na baadhi ya watu ambao wana wasiwasi zitakapoishia silaha hizo.

Wakati huo huo, Mkuu wa Baraza la Kamati ya Mahusiano ya Marekani ameiomba nchi yake kupeleka silaha Ukraine ili kukabiliana na kinachodaiwa uvamizi unaofanywa na Urusi. Robert Menendez amesisitiza Umoja wa Ulaya kutoa silaha za kivita kuisaidia Ukraine ili iweze kujihami dhidi ua Urusi.

Wito huo umekuja huku Rais Putin wa Urusi akiita majadiliano ya haraka kuhusiana na mwa Ukraine kama nafasi ya kufanya makubaliano ya kusitisha uhasama wao. Kauli ya Putin inakuja ikiwa ni siku moja kabla ya mazungumzo yatakayofanyika huko Minsk kati ya Ukraine na Urusi kujadili machafuko hayo.
-BBC