Wanawake Wapewa Vyoo 108 vya Msaada India

Vyoo vilivyotolewa kwa msaada nchini India.

Vyoo vilivyotolewa kwa msaada nchini India.

KIKUNDI kimoja cha kujitolea nchini India kimegawa vyoo 108 bure katika Kijiji cha Katra Sahadatganj ambako wasichana watatu waliuawa kwa kunyongwa katika miti mwezi Mei mwaka 2014 wakitafuta sehemu ya kujisaidia porini.

Mei 2014 wasicha watatu ndugu waliuwa katika eneo la Katra Sahadatganj huko Uttar Pradesh wakati walipokwenda kujisaidia porini. Wanaharakati waliliona hilo la uhaba wa vyoo ambalo liliwalazimu wasicha na wanawake kutembea umbali mrefu ili kujisaidia na ndiko huko hukumbwa na masahibu.

Nusu ya watu nchini India sawa na watu bilioni 1.2 hawana vyoo vya kujihifadhi. Wananchi walisema kupatikana kwa msaada huo wa vyoo itakuwa nafuu hivyo hakuna mwanamke ambaye atapoteza uhai ati tu kaenda haja.ni kauli ya Bindeshwar Pathak, mvumbuzi wa vyoo hivyo nafuu.
-BBC