MSANII nyota wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Nasib Abdul aka Diamond Platnumz juzi (Agosti 30, 2014) alijikuta akiokolewa na polisi wa nchini Ujerumani asile kichapo toka kwa mashabiki wenye hasira kwenye ‘show’ yake baada ya kuwaudhi mashabiki hao.
Katika onesho hilo Diamond lililofanyika mjini Stuttgart, Ujerumani, mashabiki waliokuwa na hasira walikerwa na kitendo cha wao kumsubiri msanii huyo tangu saa nne usiku hadi saa 11 asubuhi. Inadaiwa kuwa mashabiki hao waliokuwa wametozwa kiingilio cha euro 25 kwa kila mtu na walijulishwa kuwa show ingelianza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 usiku au alfajiri ndipo Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake Awin Williams Akipomiemie raia wa Nigeria.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki kwa kudanganwa hivyo kuanza kurusha chupa huku wakitaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake wampe kichapo. Hata hivyo kilichowakera zaidi mashabiki ni tukio la vyombo vibovu vya muziki vilivyofungwa katika ukumbi huo na kuwa na kero mara kadhaa kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvamia na kuvunja hadi vyombo vya muziki na kutoa kichapo kwa ma-Djs ambao walilazimika kukimbizwa hosptalini baada ya kipigo.
DJ Drazee alijikuta akila kichapo kutoka kwa mashabiki hadi kukimbizwa hospitalini huku mmoja wa Djs hao akipoteza Laptop yake na DJ Flor kupatwa mstuko wa moyo na kulazimika pia kukimbizwa hosptalini.
Polisi nchini Ujerumani ambao walimuokoa Diamond wanasema tukio hilo halijawahi kutokea na ni la aibu kutokea, kwa msanii kuchelewa jukwaani kwa nchi kama Ujerumani, jambo ambalo ni la hatari kwani mashabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao. Hadisasa Polisi wanamsaka mwandaaji wa onesho hilo na walisema wanachunguza hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na itamfungulia mashataka muandaaji wa onesho, Williams Akpomiemie.