Je, Kwanini Wanawake Husifika kwa Vitendo vya Ukatili?

Moja ya kitendo cha ukatili kilichofanywa na mwanamke baada ya kujifungua na kutupa kiumbe hiki. dev.kisakuzi.com inaomba radhi kwa picha hii ya kikatili.

Moja ya kitendo cha ukatili kilichofanywa na mwanamke baada ya kujifungua na kutupa kiumbe hiki. dev.kisakuzi.com inaomba radhi kwa picha hii ya kikatili.


Na Happy Joseph
NIMEJARIBU kuchambua kwa kadri nilivyoweza na kwa ufupi(japo haitaonekana kama uchambuzi mfupi)
Matukio ya kinyama kwa ujumla wake bila kuseparate jinsia yanasababishwa na kitu kimoja kikubwa…KUKOSA UPENDO.
Nadhani kukosa upendo kwaweza kutazamwa zaidi kiimani na kisaikolojia.
KISAIKOLOJIA
Binadamu tangu atungwapo mimba huanza kujifunza na kujenga tabia yake atakayokuwa nayo siku za baadaye. Wataalam wa saikolojia wanasisitiza mama mjamzito kuwa makini sana kwa kuwa hali yake(hasira, afya, nk) hupredict physical appearance and psychological development ya mtoto. Mf, mama anapokosa huduma bora za afya na chakula, kiumbe aliye tumboni huathirika…au ikiwa mama atapigwa within the first three months za ujauzito, kuna possibility mtoto akazaliwa na ulemavu(miezi mitatu ya mwanzo ni sensitive kwa kuwa sells zinajigawanya kuunda mwili wenye viungo vya binaadam, na ikiwa kutakuwa na disturbance yoyote kunaweza kuathiri hatua hii muhimu~IELEWEKE KUWA abnormality ya mtoto atakayezaliwa kwa madhara haya haina uhusiano na ile ya kurithi~)
Wataalam wanashauri mama kupata treatment nzuri toka kwa wanafamilia na jamii zitakazomfanya awe comfortable kipindi chote cha ujauzito, hatimaye kujifungua mtoto mwenye afya na ukuaji mzuri kisaikolojia. Pia mama anapopata hasira, au chuki kipindi cha ujauzito hasa zenye connection na ujauzito alionao(Mf, mimba isiyotarajiwa, ujauzito utokanao na kubakwa) humuathiri kisaikolojia kiumbe aliye tumboni
Swali: Wanawake wangapi wanaopata huduma stahiki zitakazowawezesha kuzaa kiumbe bora?~Wachache sana: hivyo watt wengi huzaliwa wakiwa wameathirika kisaikolojia(kundi hili tunakutana na watoto wenye chuki, hasira, kuburi nk)
KIIMANI
Kukosa upendo kunaanza tangu kutungwa mimba.
Mazingira ya utungwaji mimba ni mwanzo wa safari ya kiumbe kipya.
Ikiwa mimba si ya kutarajiwa(hata kama ni ndani ya ndoa)wazazi HUICHUKIA ile mimba(ikizingatiwa hakuna means yoyote ya kufanya abortion~illegality ya utoaji mimba…. na dhana ya mauaji ya kiumbe kiimani)
Hivyo mama analazimika kulea mimba asiyoitaka. Connection ya mama na mtoto ni ya ajabu sana, mama anapokuwa na furaha, mtoto aliyeko tumboni naye huwa na furaha (you can feel it kicking happily) na vilevile kinyume chake.
Chuki kwa ujauzito huunda roho ya chuki kwa kiumbe aliye tumboni na kiumbe huyu hujijengea kuwa huu ndio utaratibu…. meaning ndio maisha…
Mtoto anazaliwa akiwa hana roho ya upendo….
Maswali: je, mimba ngapi zinatungwa kwa kutarajiwa~chache sana
Je,mimba ngapi zinakataliwa na mzazi wa kiume? ~Nyingi sana~
SAFARI YA MAISHA BAADA YA MTOTO KUZALIWA.
Baada ya mtoto kuzaliwa (spiritual and psychological abnormal) chuki iliyojengwa akiwa mimbani hukuzwa ama kufifishwa na mapokezi ya mtoto, malezi pamoja na mazingira….
Mtoto aliyezaliwa pasipo kuhitajika (mtoto aliyetungwa kwa ubakaji, mimba shuleni, kabla ya wakati uliopangwa na wanandoa) namna alivyopokelewa katika family na jamii (mara nyingi hapendwi kama wenzake) humfanya ajijengee dhana kuwa the world is unfair….comparing him/herself with other kids.
Utashangaa mtoto mdogo anapiga wenzake kama vile hana akili nzuri…..(hata kama mazingira aliyokulia HAKUNA vitendo vya kupiga ambavyo unaweza kusema kajifunza)
Pamoja na kuwa mtoto katika umri wa miaka 2-6 huwa egocentric~mbinafsi~ hasa katika kutaka kujimilikisha vitu vyake, bado hakumfanyi awe na CHUKI kiasi cha kupiga wenzake mara kwa mara….na mara nyingi watoto hawa walioathirika kisaikolojia, huwa hawana furaha, hujitenga na wenzao, huwa na kiburi, si wasikivu na hulalamika kutotendewa haki…. hata kama wametendewa haki… Chuki hii ni zaidi ya ubinafsi ambao ni normal…. chuki hii ni hatua mojawapo ya ku~reveal what embodies his/her behaviour.
Ikiwa mzazi ataendeleza chuki yake kwa mtoto huyo, ajue wazi kuwa anajenga tabia au roho ya chuki kwa mtoto na ndivyo atakavyoishi
Kuna dhana kuwa, wazazi wenye watoto wengi wasiowamudu huchangia kujenga tabia ya chuki kwa watoto wao.
Mara nyingi katika familia hizi kubwa, wazazi huelekeza mapenzi kwa watoto wawili au mmoja na kuwafanya wengine wajisikie kuwa wao si sehemu ya familia hivyo basi kutokuwa na upendo kwa wengine
HATUA YA UTU UZIMA
Katika dunia hii yenye kila aina ya challenge watoto wengi wamezaliwa na kukulia katika mazingira yasiyo na upendo….
Jambo hili linaathiri sana tabia zao, hasa MAHUSIANO YAO NA WENGINE…..wanaoathirika zaidi ni WANAWAKE
SABABU:
1. Wanawake wana majukumu mengi tangu wakiwa watoto~ikizingatiwa kuwa katika jamii nyingi mwanamke ndiye muwajibikaji mkuu katika shughuli mbalimbali(utotoni watoto wa kiume hawapewi kazi nyingi kama wale wa kike) hivyo watoto wa kike hujenga chuki dhidi ya unequal treatment za namna hii
2. Pamoja na mchango mkubwa wa wanawake katika jamii, bado thamani yao imewekwa chini ya kiatu jambo ambalo huongeza chuki ya mwanamke dhidi ya jamii(hasa ikizingatiwa hakuna anayejali hata wanawake wakipiga kelele zote)
3. Mwanamke huishi maisha ya hofu dhidi ya vitendo vya kinyama (sexual harassment) zinazomfanya aishi maisha ya kutaka kulipiza kisasi
Zipo sababu nyingi, ila lazima tujue kwa nini watoto ndio wanaoathiriwa zaidi na chuki ya mwanamke
~mwanamke atamyanyasa mtoto wa kambo kwa kuwa anadhani kuwa mtoto yule kapewa thamani kubwa kuliko wake aliowazaa. Na kama hana mtoto hapo chuki huwa kubwa zaidi kwa kuwa anaona hakuwa treated fairly…. hasa baada ya kuwa na tatizo la ugumba.
~watoto wana usumbufu wao(hata wale wa kuwazaa) hivyo hasira katika mambo mengine kunamfanya mama huyu kuzihamishia zoooooote kwa mtoto (ambaye ni easy target)……kama vile mwalimu ahamishavyo hasira za nyumbani kwake kwa wanafunzi….
~majukumu huleta uchovu ambao kila mtu anahitaji faraja…. mwanamke ambaye alibakwa akapata mimba, au katika mahusiano alipata ujauzito kisha ukakataliwa, hicho kiumbe kiko hatarini sana kwa kuwa chuki ya mwanamke ni nzito…. mwanamke anapokuwa broken hearted, hasira na chuki yake ni kuu kiasi cha kuweza kuuondoa uhai wa mtu..(hili ni jambo la kawaida kimaumbile…..mwanamke kaumbiwa huruma kuu na mbadala wa huruma hiyo ni chuki kuu….) hivyo basi, kama majukumu ya malezi kaachiwa, jamii inamtazama kwa jicho la malaya…..Aliyekuzalisha anakutazama kwa jicho la takataka…..
Bado unahitaji kujitunza na kutunza kiumbe ulichoachiwa hasira zooooooote zinahamishiwa kwa mtoto….
Si busara ila lazima ifahamike kuwa si wote wanaoweza kutuliza hasira zao bila kufanya jambo baya
Nadhani mwanamke ni kiumbe sensitive sana, anahitaji support ya kutosha pale anapopatwa na janga. Na pia anahitaji sana ushauri katika kufanya maamuzi hasa nyakati anapoumizwa,
Nashauri, kuwe na seminars toka kwa wataalamu wa kisaikolojia na kiimani katika jamii zetu ili kupunguza matukio ya kinyama yanayoweza kutokea
Imeandaliwa na Happy Joseph