MAJESHI ya Marekani yameendelea kuwashambulia wapiganaji wa Islamic State (IS) nchini Iraq licha ya vitisho kutoka kwa kundi hilo kuwa watawaua mateka wengine Wamarekani iwapo Obama angeendelea kuishambulia himaya hiyo Kaskazini mwa Iraq.
Majeshi ya Marekani kwa kushirikiana na ndege maalum za kivita zisizokuwa na rubani zilifanya mashambulizi 14 usiku wa kuamkia jana. Mashambulizi hayo 14 ya angani yamefanyika katika eneo karibu na bwawa la Mosul na yalilenga kuwasaidia wanajeshi wa Iraq na wa kikurdi.
Maofisa wajeshi la Marekani wamesema kuwa walifaulu kulipua magari ya kijeshi na vitu vingine vilivyokuwa vikitumiwa na wapiganaji wa IS. Tarifa kutoka kwa wakurdi zinasema kuwa ndege ambazo hazina rubani zilikuwa angani kuwalinda wanajeshi Wakurdi wakati wapiganaji wa Pesh Merga wakisukumwa katika milima, kusini mashariki mwa bwawa kubwa la Mosul, ambalo lilitwaliwa tena kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu wiki hii.
Pentagon imethibitisha kuwa mashambulizi kumi na manne ya angani yalifanywa katika sehemu hiyo kuliko bwawa na kuyalenga magari kadhaa ya kijeshi na vitu vingine. Televisheni ya taifa ya Iraq imesema kuwa ndege hizo za vita za Marekani zilikuwa pia zimetekeleza mashambulizi katika kambi za magaidi mkoani al-Anbar hadi magharibi mwa Baghdad, na zilikuwa zimetoa ulinzi wa angani kwa vikosi vya serikali vilivyokuwa vikielekea kuwakabili waasi wa kisuni.
Majeshi ya Marekani yameendelea kuwashambulia wapiganaji wa Islamic State huko Iraq licha ya vitisho kutoka kwa kundi hilo kuwa watawaua mateka wengine wamarekani iwapo Obama angeendelea kuishambulia himaya hiyo kaskazini mwa Iraq. Majeshi ya Marekani kwa ushirikiano na ndege zisizikuwa na marubani zilifanya mashambulizi 14 usiku.
Mashambulizi kumi na manne ya angani yamefanyika katika eneo karibu na bwawa la Mosul na yalilenga kuwasaidia wanajeshi wa Iraq na wa kikurdi.
-BBC