Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Merry Nagu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya Wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na watoa huduma sekta ya fedha. Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza na vyombo vya habari kuelezea umuhimu wa semina ya Wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na watoa huduma sekta ya fedha iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kwenye Hoteli ya Serena.
Asia Natalia Mhina Meneja wa Biashara ya M-Pesa kutoka kampuni ya Vodacom akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya semina ya Wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na watoa huduma sekta ya fedha kufunguliwa. Semina hiyo maalum imeandaliwa na Taasisi ya Sekta bianfsi Nchini (TPSF) na kufadhiliwa na makampuni ya Vodacom na FSDT.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Godfrey Simbeye (kulia) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Merry Nagu (wa pili kushoto) mara baada ya kufungua rasmi semina ya Wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja waliokutana na watoa huduma sekta ya fedha. Wa kwanza kushoto ni Rais wa VICOBA Endelevu, Bi. Devota Likokola (Mb).
Meza kuu katika semina ya Wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na watoa huduma sekta ya fedha. Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Semina hiyo maalum imeandaliwa na Taasisi ya Sekta bianfsi Nchini (TPSF) na kufadhiliwa na makampuni ya Vodacom na FSDT.
Baadhi ya washiriki wa semina ya Wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na watoa huduma sekta ya fedha wakifuatilia mada katika semina hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Semina hiyo maalum imeandaliwa na Taasisi ya Sekta bianfsi Nchini (TPSF) na kufadhiliwa na makampuni ya Vodacom na FSDT.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Merry Nagu akibadilishana mawazo na baadhi ya baadhi ya washiriki wa semina ya Wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na watoa huduma sekta ya fedha mara baada ya kufungua semina hiyo leo.
Picha ya pamoja kati ya washiriki wa semina ya Wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na watoa huduma sekta ya fedha iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Semina hiyo maalum imeandaliwa na Taasisi ya Sekta bianfsi Nchini (TPSF) na kufadhiliwa na makampuni ya Vodacom na FSDT.