Serikali Ngorongoro Yatakiwa Kutoa Ushirikiano kwa Redio za Kijamii

Wanakikundi cha ngoma na wakazi wa kata ya Ololosokwani wakiangalia taarifa mbalimbali za mitandao kwenye “Tablet” inayotengenezwa na kampuni ya Samsung wakati wa ziara hiyo

Wanakikundi cha ngoma na wakazi wa kata ya Ololosokwani wakiangalia taarifa mbalimbali za mitandao kwenye “Tablet” inayotengenezwa na kampuni ya Samsung wakati wa ziara hiyo

wakipata mafunzo

DSC_0010

Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwakaribisha wadau wa maendeleo ofisini kwake Loliondo walioongozwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa tatu kushoto) aliyefuatana na Meneja Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania , Bw. Slyvester Nteere (wa pili kushoto) pamoja na mwakilishi wa Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Eric Kalunga (kushoto) wakiwa na mwenyeji wao Diwani wa kata ya Ololosokwani, Yannick Ndoinyo (kushoto kwa DC).

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro

Serikali na halmashauri wilayani Ngorongoro zimetakiwa kutoa ushirikiano kwa redio za kijamii wilayani humo kwa lengo la kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi wao.

Hayo yameelezwa na Meneja wa redio ya kijamii ya Loliondo FM, Joseph Munga, wakati wa ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) redio hiyo ikiwa miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO wilayani hapa wakiambatana na wadau wa maendeleo kutoka kampuni ya Samsung na Ubalozi wa Uswiss hapa nchini.

‘Redio za Jamii ndio chombo pekee kinachoziunganisha serikali na jamii katika suala zima la kujiletea maendeleo’ alisema Joseph Munga.

DSC_0019

Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwa kwenye mazungumzo na wadau wa maendeleo waliofika wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Munga aliongeza kwa kusema kuwa redio hiyo iliyoanza kurusha matangazo mwezi Oktoba 2013 imekuwa ni kichocheo cha kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii wilayani Loliondo na kuibua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii huku akiitaka serikali na halmashauri wilayani humo kuisaidia katika kufikia malengo ya kuitumikia jamii na kuwashukuru wadau mbali mbali wanaoiwezesha redio hiyo ikiwemo kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambayo imetoa mnara wao kurushia Matangazo ya redio Loliondo.

“Suala hapa ni ushirikiano hasa kwa halmashauri kuelewa na kuona umuhimu wa kutumia redio hii katika matukio mbali mbali yanayofanyika kwenye halmshauri vikiwemo vikao vya baraza la madiwani ili wananchi walioshindwa kufika waweze kujua baraza lao limepitisha nini sanjari na huduma kwenye sekta za afya na elimu”, alisema Munga.

Redio Loliondo ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO wilayani humo kupitia asasi isiyokuwa ya kiserikali ya RAMAT kwa kufadhili miradi ya Maktaba,kutoa elimu kwa jamii ya kifugaji yenye malengo ya kuinua uelewa na ufahamu kwa jamii hizo zilizopo pembezoni hasa katika suala zima la kujiletea maendeleo.

DSC_0049

Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kushoto) ambaye pia ndio mkuu wa msafara huo akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo hayo. Kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania, Bw. Slyvester Nteere.

Nae Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, alisema kuwa misingi ya redio hiyo inalenga kuikomboa jamii ya Loliondo kwa kutoa elimu ya kifugaji na elimu kwa wananchi wilayani humo ambao hapo awali hawakupata fursa ya kupata taarifa na matukio mbalimbali yanayoendelea wilayani humo.

Akifafanua faida za redio hiyo kwa jamii ni kupata taarifa mbali mbali zinazoendana na shughuli zao za ufugaji hususan taarifa za chanjo ya mifugo na madawa na kupata taarifa nyingine kuhusiana na masuala mbali mbali ya kijamii ndani na nje ya wilaya hiyo ambayo hapo awali yalikuwa vigumu kupatikana kwa wakati kutokana na jiografia ya wilaya hiyo.

“Pamoja na kwamba malengo ya mradi huu yameanza kuonekana dhahiri machoni petu,wafadhili kutoka UNESCO pamoja na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ambayo mnara wake umekuwa ukitumika kurusha matangazo ya redio hii, tunataka kuhakikisha kwamba mnaweza kujiendesha wenyewe hapo baadae ili mradi kama huu uweze kuwanufaisha na wenzenu sehemu zingine”, alisema Al Amin.

DSC_0156

Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maelezo juu mradi waliobuni wa kituo cha utamaduni wa Kimasai ambao uko mbioni kuanza ujenzi wake wakati wa ziara ya UNESCO kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika hilo.

Akizungumzia miradi inayoletwa na wafadhili wilayani humo Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alisema kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa kuwahamasisha vijana ambao wana shauku ya kuishi mijini kurudi nyumbani na kuendeleza jamii hali ambayo imetafsiriwa kutoa uelewa kwa wanajamii na hivyo ni faraja kubwa kwa wananchi wilayani Loliondo.

Ameyataka mashirika na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kuingalia Ngorongoro kwa ukaribu na kuwa wadau wazuri wa kuiletea maendeleo wilaya hiyo kwani miradi iliyopo itachochea ukuaji wa uchumi na kusaidia uelewa wa wakazi wilayani Loliondo katika dhana nzima ya kujileta maendeleo na kukuza uelewa wa wananchi wa kupata taarifa mbalimbali kwa wakati.

DSC_0179

 

Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili lulia) akitoa ushauri kuhusu kituo hicho kuwa kitakuwa na manufaa ya kiuchumi kwa jamii hiyo ya kifugaji pindi kitapokamilika huku akisisitiza kuwa mipango iliyopangwa kama walivyopewa maelezo iendane na wakati.

DSC_0310

Mmoja wa wadau wa maendeleo kutoka Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Erick Kalunga akisoma moja ya vitabu ndani ya maktaba hiyo inayofadhiliwa na UNESCO, Maktaba hiyo inayotumiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Ololosokwani na vijana wa kata hiyo.

DSC_0361

Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) ambaye pia ni mkuu wa msafara huo wa kukagua miradi inayofadhiliwa na UNESCO akiteta jambo na Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere ndani ya maktaba hiyo. Anayefuatilia mazungumzo hayo kwa karibu ni Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (katikati).

DSC_0294

Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) akitoa maelezo baada ya kutembelea Maktaba inayofadhiliwa na UNESCO nje ya maktaba hiyo.

DSC_0392

Kikundi cha ngoma ya Kimasai kilichowatumbuiza wageni waliotembelea mradi wa redio ya Loliondo FM inayofadhiliwa na UNESCO wakitumbuiza wakati wa ziara hiyo.

DSC_0412

Afisa Miradi wa kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko, akijumuika na kinamama wa kikundi cha ngoma za kimasai kutoka kata ya Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

DSC_0432

Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ikiwemo maktaba, redio na ugawaji wa vitabu vya masomo ya Sayansi na hesabu vinavyoafadhiliwa na UNESCO kwenye kata hiyo.

DSC_0441

Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akitoa pongezi kwa redio Loliondo FM kwa kuweza kuihamasisha jamii inayoizunguka kwa kuburudisha, kutoa elimu na habari kwa ujumla hiyo sio kazi nyepesi kutokana na uchanga wenu wa redio yenu.

DSC_0476

Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akikabidhi zawadi kwa kikundi cha ngoma cha kinamama wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi inayofadhiliwa na UNESCO kwenye kata ya Ololosokwani.

DSC_0478

Wanakikundi cha ngoma na wakazi wa kata ya Ololosokwani wakiangalia taarifa mbalimbali za mitandao kwenye “Tablet” inayotengenezwa na kampuni ya Samsung wakati wa ziara hiyo.

DSC_0488

Mmoja wa wanakikundi akitumia Tablet kupiga picha wanakikundi wenzake pamoja na wadau wa maendeleo (hawapo pichani).

DSC_0509

Wanakikundi cha ngoma za kimasai wakiwa kwenye picha ya pamoja na ugeni huo huku wakionyesha furaha baada ya kupokea zawadi ya fulana kutoka kampuni ya Samsung.

IMG-20140807-WA0024

Meneja wa redio jamii ya Loliondo FM, Joseph Munga akiwa kwenye studio za redio hiyo wakati wa ziara ya UNESCO kukagua miradi inayoifadhili.

DSC_0516

Meneja mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere (aliyeketi) akiwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph ndani ya studio za kurushia matangazo za redio ya Loliondo FM inayorusha matangazo yake kwenye mnara wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kuifika jamii kubwa kwenye maeneo hayo.