Mfuko wa LAPF Waanza Kutoa Mikopo ya Elimu ya Juu…!

Afisa matekelezo wa LAPF  Bi Christina Mbaga akitoa maelezo juu ya Mkopo wa Elimu unaotolewa kwa wanachama wa LAPF. Mkopo huu umekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na wasio wanachama.

Afisa matekelezo wa LAPF Bi Christina Mbaga akitoa maelezo juu ya Mkopo wa Elimu unaotolewa kwa wanachama wa LAPF. Mkopo huu umekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na wasio wanachama.

 Kaimu Meneja Masoko wa LAPF, Bi. Rehema Mkamba akitoa maelezo kwa wananchi na wanachama waliotembelea banda la LAPF Nane Nane Mjini Dodoma.
 
Ofisa Mifumo ya Computer wa LAPF, Bi. hilda Kato akifafanua jambo kwa wanachama waliotembelea bandani hapo. 
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF walioshiriki katika maonyesho ya Nane Nane Nzuguni Mjini Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja. Mfuko wa Pensheni wa LAPF umeanza kutoa Mikopo ya Elimu ya Juu kwa wanachama wake kwalengo la kuwasaidia wanachama wanaotaka kujiendeleza kielimu kwa kuwalipia ada ya masomo. LAPF inajua kuna baadhi ya wanachama walitamani kujiendeleza kielimu lakini kwa namna moja au nyingine wameshindwa kutokana na gharama za masomo hayo hivyo LAPF itawawezesha kutimiza malengo yao.  LAPF ndio Mfuko Pekee wa Pensheni nchini unaotoa mkopo wa Elimu kwa wanachama wake. 
LAPF, MCHANGO ULE ULE MAFAO ZAIDI.