Pilipili, Omondi na Anne Kansiime Jukwaa Moja Augost 2

Mchekeshaji ajulikanae kwa jina la kisanii wa Nchini Tanzania, Mc Pili Pili akitoa vibwagizo vya uchekeshaji kwenye mkutano wa waandishi wa habari  uliofanyika 1 Agosti 2014 jijini Dar es Salaam kuhusina na maandalizi la onesho la vichekesho litakalofanyika kesho Agosti 2,2014  katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis,ambaye ndio waandaaji wa Onesho hilo, Mchekeshaji kutoka nchini Uganda,Anne Kansiime (wa pili kulia), Kushoto kwake mchekeshaji kutoka nchini Kenya,Fred Omondi.

Onyesho la Uchekeshaji linalowakutanisha wasanii wa tasnia hiyo kutoka nchi za Jumuhia ya Afrika mashariki Tanzania, Kenya na Ugana linatarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika Ukumbi wa Golden Tulip Jijini Dar es salaam, Wasanii hao ambao ni kivutio kwa mashabiki katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki wamewasili nchini na kupokewa na mashabiki pamoja na wenyeji wao.

MC Pilipili akitoa neno

MCPilipili akitoa neno

Akiongea mchekeshaji Anne Kansiime anasema kuwa anatarajiwa kutoa burudani siku ya Jumamosi kwa mashabiki wake katika ukumbi wa Golden Tulip.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, mkali huyo wa kuchekesha na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo Jumamosi.

‘Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.

Kwa upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred Omondi, amesema watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka Kwa Nguvu.

‘Usiku wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.

Naye mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku wa kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.Usiku wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani waliyowaandalia. ‘Usiku huo utakuwa ni maalumu kwa watanzania kufurahia Utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert.

Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.

Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.