ZAIDI ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini India, huku 20 wakithibitika kufariki dunia katika Kijiji cha Malin karibu na Mji wa Pune lilikotokea janga hilo. Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
Vikosi vya uokoaji vimeendelea na kazi ya kuwanusuru waliofukiwa na maporomoko ya udogo, japo kuwa mazingira magumu na hali mbaya ya hewa vinakwamisha shughuli hiyo. Maporomoko hayo yaliyokikumba kijiji cha Malin India karibu na jimbo la Maharashtra yamesababisha nyumba nyingi kusombwa huku watu wakihofiwa kunaswa pia katika eneo hilo.
Mwandishi aliyepo katika eneo la tukio anasema jengo pekee linaloonekana kunusurika na janga hilo ni la shule, huku maeneo mengine yakiwa tambarale kabisa. Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi amesema maporomoko ya ardhi ni jambo la kawaida kutokea nchini humo hasa kipindi cha mvua zitokanazo na pepo za Monsoon ambazo hunyesha kuanzia June hadi Septemba kila mwaka. Hivyo wanachukua hatua kuokoa waliapatwa na maafa hayo.
-BBC