Ajali ya Basi la Morobest na Rori Yaua 17 na Kujerui 56

Pichani juu ni matukio ya picha baada ya ajali ya basi la Morobest namba T258 AHV lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam na Lori namba T820CKU na tela namba T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.Pichani juu ni matukio ya picha baada ya ajali ya basi la Morobest namba T258 AHV lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam na Lori namba T820CKU na tela namba T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Pichani juu ni matukio ya picha baada ya ajali ya basi la Morobest namba T258 AHV lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam na Lori namba T820CKU na tela namba T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Pichani juu ni matukio ya picha baada ya ajali ya basi la Morobest namba T258 AHV lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam na Lori namba T820CKU na tela namba T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.


WATU 17 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 56 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Morobest namba za usajili T258 AHV lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam na Lori namba T820CKU na tela lake namba T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma inaeleza ajali hiyo imetokea Julai 30, 2014 eneo la Pandambili barabara ya Dodoma – Morogoro majira ya saa 08:00 asubuhi. Taarifa zinaeleza kuwa basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Said Lusogo huku dereva wa lori akiwa Gilbert Isaya Nemanya ambao wote wamefariki dunia katika ajali hiyo.

“…Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na dereva wa lori hilo pamoja na utingo wake. Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita (overtake) gari lingine na kwenda kuligonga busi hilo,” inaeleza taarifa hiyo