Makamu wa Rais Dk Bilal alipohudhuria hafla ya Kilimo Kwanza


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya Tela la Trekta linalotengenezwa nchini, wakatiti wa wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.


Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo kuhusu matumizi ya Trekta dogo la mkono (Power Tila) linalotumika kwa Kilimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi funguo ya Trekta la kilimo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Teresia Huvisa, kwa ajili ya matumizi ya kilimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwalimu wa Shule ya Msingi Bwigiri ya Wasioona, Achimpota Nicolaus na kumtazama mmoja wa wanafunzi wasioona, Hasanat Athuman, kuhusu jinsi wanavyowafundisha wanafunzi wasioona, wakati alipotembelea katika Banda la Wilaya ya Chamwino kwenye maonyesho maadhimisho ya sikukuu ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.


Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Kilimo na Mbogamboga na Matuda, Hery Ndumukwa, kuhusu zao la Nyanya.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akijaribu kubeba shina la Muhogo, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika viwanja vya Nzuguni Nane Nane mjini Dodoma leo Agosti 03, 2011. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR.