JESHI la Cameroon limesema kuwa kundi la wapiganaji Waislamu la Nigeria, Boko Haram, limemteka nyara mke wa Naibu wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ambaye pia ni mwanasiasa mashuhuri kaskazini mwa nchi hiyo.
Mke wa Naibu Waziri Mkuu, Amadou Ali, na msaidizi wake wa nyumbani, walitekwa katika Mji wa Kolofata, karibu na mpaka wa Nigeria. Taarifa zaidi zinasema kuwa mapigano baina ya Boko Haram na wanajeshi wa Cameroon yanaendelea.
Boko Haram imefanya mashambulio kadha kaskazini mwa Cameroon; na mwishoni mwa juma wafuasi zaidi ya 20 wa Boko Haram walifungwa nchini Cameroon baada ya kukutikana na hatia ya kupanga mashambulio kadhaa.
-BBC