Ofisa Mfuko wa Hiari wa Kujiwekea akiba uzeeni (GEPF), Aziza Selemani akitoa ufafanuzi kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya Wakulima ya Nane nane jana mjini Dodoma.
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha Eva Varelian (kushoto) na Alice Kihiyo (kulia) wakimhudumia mteja jana mjini Dodoma wakati wa maonyesho ya nane nane yanayoendelea.
Ofisa Uhisiano wa Mfuko wa Penseni wa PPF, Edward Kyungu akitoa maelezo kwa mwananchi katika banda la Wizara ya Fedha jana juu ya muhimu wa mfuko huo katika maonesho ya wakulima ya nane nane yanaoendelea mjini Dodoma.
Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma (kulia) akibadilishana mawazo na Onni Sigara (katikati) na Adamu Msumule (kushoto) jana kwenye maonesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea mjini Dodoma.
Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta kutoa Wizara ya Fedha, Elimu Sekeni akitoa maelezo kwa wadau anuai waliotembelea banda lao jana mjini Dodoma juu ya mifumo ya kompyuta na mishahara ya Serikali kwenye maonesho ya wakulima nane nane.