Ndege ya Malaysia Yaanguka, Yaua Abiria 295

Ndege ya Malaysia namba MH17 ikiteketea baada ya kuanguka.

Ndege ya Malaysia namba MH17 ikiteketea baada ya kuanguka.

Ndege ya Malaysia namba MH17 ikiteketea baada ya kuanguka.

Ndege ya Malaysia namba MH17 ikiteketea baada ya kuanguka.

NDEGE ya Shirika la Ndege Nchini Malaysian ikiwa na abiria 295 imeanguka Mashariki mwa Ukraine ikiwa safarini kutoka Amsterdam, Uholanzi kuelekea Kuala Lumpur na kuua abiria wote. Taarifa za awali zinasema ndege hiyo imedunguliwa ikiwa angani.

Taariza zaidi zinasema miili ya watu imetapakaa kila upande karibu na Kijiji cha Grabovo, eneo ambalo linadhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga. Ndege hiyo aina ya JET namba MH17 ilikata mawasiliano ikiwa inakaribia kuingia anga ya Urusi.

Rais wa Ukraine ameelezea tukio hilo kuwa ni tendo la kigaidi huku waasi wakikanusha kuidungua ndege hiyo kama inavyodhaniwa. Inaaminiwa waasi hao wanaotaka kujitenga walizidungua ndege mbili za jeshi la Ukraine katika eneo hilo hivi karibuni. Anga ya Ukraine haikufungwa rasmi lakini mashirika ya ndege ya Ujerumani, Lufthansa, Air France ya Ufaransa na Uturuki, yanaliepuka eneo la Ukraine Mashariki.