Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana akikabidhiwa Kitambulisho chake na Ofisa Usajili Wilaya ya Kinondoni, Abdulrahman Muya baada ya kukamilisha hatua za mwisho za uhakiki Kata ya Saranga Mbezi Dar-es-Salaam. Kushoto ni Bw. Dickson Mbanga Weiss, Ofisa Usajili Kinondoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana akimkabidhi mmoja wa wananchi, Bi. Chiku Issa Waziri kitambulisho cha Taifa, akishuhudiwa na maofisa usajili katika wilaya, Dickson Mbanga Weiss na Abdulrahman Muya
Mmoja wa wananchi wa Kata ya Saranga akiongozwa na Ofisa Usajili wa NIDA kukamilisha hatua za mwisho za kuhakiki taarifa zake kabla ya kukabidhiwa kitambulisho chake, Kata ya Saranga Mbezi.
1. Mkuu wa Wilala ya Kinondoni akiwasili katika Kata ya Saranga Mbezi tayari kuzindua zoezi la utoaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Kata ya Saranga, Mbezi Dar-es-Salaam.
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kutoa vitambulisho vya taifa rasmi kwa wananchi wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa vitambulisho hivyo limefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana ambaye alianza kwa kupokea kitambulisho chake na pia kuwakabidhi wananchi 22 vitambulisho vyao wa kutoka Kata ya Saranga Mtaa wa Matangini.