Serengeti Boyz Kujipima Azam Complex

Uwanja wa Azam Complex

Uwanja wa Azam Complex

TIMU ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boyz) inacheza mechi ya kujipima nguvu Julai 11 mwaka huu dhidi ya Azam U-20 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Mechi hiyo ambayo ni maalumu kwa benchi la ufundi la Serengeti Boyz likiongozwa na kocha Hababuu Ali Omari kuangalia kikosi chao itaanza saa 2 kamili asubuhi.
 
Serengeti Boyz itacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) siku ya Ijumaa, Julai 18 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Azam Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.
 
Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boyz ni Abdallah Shimba, Abdulrasul Bitebo, Abutwalibu Mshery, Adolf Bitegeko, Ally Mabuyu, Ally Mnasi, Amin Noren, Athanas Mdamu, Badru Othman, Baraka Baraka, Hatibu Munishi na Issa Athuman.
 
Wengine ni Juma Yusuf, Kelvin Faru, Kelvin Kamalamo, Martin Luseke, Mashaka Ngajilo, Mechata Mnata, Mohamed Abdallah, Mussa Vicent, Nazir Barugire, Omary Omary, Omary Wayne, Prosper Mushi, Seif Seif na Yahya Hafidh.