Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah (Kulia) akisalimiana na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakati alipotembelea banda la PPF kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya sabasaba.
Ofisa Huduma Kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mohamed Siaga (kulia) akimuelezea Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka jinsi mteja anayejiunga kwa mara ya kwanza na Mfuko wa PPF kuwa pindi anapomaliza kujaza fomu yake tu hupatiwa kitambulisho chake hapo hapo.
Ofisa Huduma Kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mohamed Siaga (kulia) akimuonyesha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka moja ya vitambulisho vya wateja ambao wamejiunga na mfuko huo na kuweza kutolewa vitambulisho vyao papo hapo mara baada ya kumaliza kujaza fomu za kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PPF.
Ofisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo akimpa maelekezo ya namna PPF wanavyotumia michango ya Wanachama wao katika kuwekeza katika miradi mbalimbali ambayo baadhi ya miradi hiyo tayari ishaanza kufanya kazi.
Mratibu wa Ofisi za Kanda za PPF, Mbaruku Magawa (katikati) pamoja na Ofisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo (kulia) kwa pamoja wakimuonyesha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (kushoto) moja ya michoro ya Majengo yanayotarijiwa kujengwa na PPF kama moja ya uwekezaji wake katika Miradi ya Majengo ya Kisasa nchini.
Mratibu wa Ofisi za Kanda za PPF, Mbaruku Magawa (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa Majengo ya Kisasa yanayotarajiwa kujengwa na PPF kama njia moja wapo ya uwekezaji unaofanywa na Mfuko wa PPF. Picha Zote na Josephat Lukaza – Lukaza Blog