Bomu Lalipuka Tena Mgahawani Arusha, Lajeruhi Vibaya

Majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine aliyejulikana kwa jina la Deepak Gupta (25), akiwa amelazwa katika Hospitali ya Selian, Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), mara baada ya kukatwa mguu mmoja wa kushoto kutokana na kujeruhiwa vibaya na bomu.

Damu ikiwa imetapakaa eneo la tukio.

Damu ikiwa imetapakaa eneo la tukio.

Mmoja wa majeruhi katika mgahawa ujulikanao kwa jina la Traditional Indian Cusine  akipata matibabu hospitalini.

Askari wa Jeshi la Wananchi, JWTZ kitengo maalumu cha mabomu wakiwa katika eneo la tukio mara baada ya mlipuko.

Askari wa Jeshi la Wananchi, JWTZ kitengo maalumu cha mabomu wakiwa katika eneo la tukio mara baada ya mlipuko.

Bomu Lalipuka Tena Mgahawani Arusha, Lajeruhi Vibaya
TAARIFA zinasema bomu limerushwa ndani ya Mgahawa ujulikanao kama ‘Traditional Indian Cusine’ uliopo karibu na Hotel ya Gymkana jijini Arusha. Taarifa za awali zinasema zaidi ya raia nane wamejeruhiwa vibaya katika mlipuko huo na wamelazwa katika Hospitali ya Selian ya mkoani Arusha. Wengine hali zao ni mbaya na wapo katika uangalizi maalumu.

Baadhi ya waliojeruhiwa ni pamoja na majeruhi aliyejulikana kwa jina la Deepak Gupta (25), ambaye amelazwa katika Hospitali ya Selian, katika chumba cha watu mahututi (ICU). Taarifa zaidi baadaye.