Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama (wa tatu kushoto) akizungumza na mzazi aliyeambatana na watoto wake kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwa ajili ya kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini. Kushoto ni Amos Mtamba kijana mwenye fani ya uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia Mpango wa Kukuza Ajira kwa Vijana ” Kazi Njenje” na anayefuatia ni Programme Coordination Specialist wa UNAIDS, Jimmy Mbazi.
Amos Mtamba kijana mwenye fani ya uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia Mpango wa Kukuza Ajira kwa Vijana “Kazi Njenje” akieleza kwa mmoja wa wadau namna anavyofanya kazi zake za uchoraji ambapo UN imempa nafasi ya kuonyesha kuonyesha kazi zake za sanaa ya uchoraji kwenye banda hilo kwa ajili yakujitafutia soko na kuendeleza maisha yake.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akifafanua jambo kwa wageni waliofika kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Kampuni ya MeTL Group inahusika pia na masuala ya Vitenge, Khanga, Mashuka na n.k Njoo upendeze mwanamke na vitenge bora na imara kutoka MeTL Group…Sikukuu ya Eid ilee na maandalizi yawe mapema kabisa..!
Wakazi wa jiji la Dar wakivinjari ndani ya Banda la Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL Group) kujipatia mahitaji mbalimbali za bidhaa bora kabisa kwa bei nafuu msimu huu wa Sabasaba.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiangalia na kupata maelezo ya bidhaa mbalimbali kama TV, Music System, Simu za mkononi za nyingine nyingi kutoka kampuni ya LG ambapo MeTL Group ndio Authorized Dealers pekee nchini Tanzania.
Mmoja wa wateja akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wetu waliobobea wa vipozi kwenye banda letu la MeTL Group.
Watu wanatakaje kupendeza…..!! bado wewe tu hujajipatia kitenge chako na Khanga….kwa bei nafuu kabisa katika msimu wa Sabasaba.
Baadhi ya ushers wanaotohuduma kwa wateja ndani ya banda la MeTL GROUP wakipozi kwenye Big Screen ya LG inayoonyesha tangazo la bidhaa mpya ya “MO BEAUTY SOAP” ambapo Balozi wake ni mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania namba mbili JOKATE MWEGELO.
Mmoja wa kikundi cha uhamasishaji kwenye banda la MeTL Group akikata kiu yake na kinywa chenye ladha tamu kabisa ambacho kitaingia sokoni hivi karibuni “MO Portello” kinachouzwa ndani ya banda
hilo.
Aaaah kinywaji safi kabisa…sasa nimekata kiu yangu…!! Unakaribishwa na wewe pia kukijaribu kinauzwa kwa bei nzuri kabisa ya offer katika msimu huu wa Sabasaba.
Mimi napenda “MO Portello” wewe je….??
AGRO MeTL wauzaji wa Mbolea na Matrekta ya kisasa ambayo ni imara na bora kwa mazingira yetu ya Tanzania yapo kwenye banda letu…Kilimo kwanza ndio mpango mzima…!!
Mambo ya Katani yanahusika pia ndani ya banda la MeTL Group kwenye viwanja vya Sabasaba.
Mambo ya Ugali, Maandazi na bidhaa mbalimbali za nafaka zinapatikana pia bila kusahau MO SEMBE..Unga safi kabisa wa kupikia.
Mambo ya usafi pia yanahusika jamani eeeeh…Sabuni za kufulia za unga zenye kuondoa madoa sugu na uchafu wa aina zote zinapatikana pia wewe tu na pochi lako.
Watoto wakipata maelezo kutoka kwa mhudumu wa vinywaji vya MeTL Group kwenye banda letu ndani ya maonyesho ya Sabasaba.
Watoto wakipata Ukodak baada ya kuyakubali maji safi ya kunywa kwa gharama nafuu kabisa yanayotengenezwa na MeTL Group.
Kata kiu yako kwa kujichagulia kinywaji ukipendacho hapa ndani ya banda la MeTL GROUP.
Mmoja wa wateja akiangalia tangazo la bidhaa mpya ya MO BEAUTY SOAP ambapo Balozi wa sabuni hiyo ni mrembo aliyewahi kushitaji la Miss Tanzania namba mbili JOKATE MWEGELO.
Mfanyakazi wa MeTL Group akitoa maelezo ya ubora wa maji safi ya kunywa yenye viwango vya kimataifa. Unakaribishwa sana kuuliza maswali mbalimbali ndani ya banda letu.
Kikundi cha NOMA SANA Group kikitoa burudani nje ya banda la MeTL Group kuwatumbuiza wakazi wa jiji wanaotembelea maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini.