Tanzania Yaongoza Mkutano wa Kamati ya Viongozi Afrika Kuhusu Tabia Nchi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Kuhusu Tabia Nchi  ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki-moon pembeni mwa mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika mjini Malabo, Equatorial Guinea Juni 27, 2014. PICHA NA IKULU

Na Premi Kibanga, Malabo-Equatorial Guinea

NCHI za Afrika zinatakiwa kuwa na msimamo mmoja kuhusu jinsi ya kukabiliana na madhara ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa barani Afrika. Misimamo huo wa Afrika unatarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano mkubwa wa Dunia kuhusu masuala ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa unaotarajiwa kufanyika New York, Marekani Mwezi Septemba, 2014.

Akiwakilisha ripoti ya Kamati ya Viongozi wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani, tarehe 27 Juni, 2014 katika Mkutano wa Viongozi wa Afrika (AU), Rais Kikwete amesema kamati yake inataka kujikita na kujihusisha na masuala yanayohusu fedha na teknolojia, hatua za kupunguza madhara, na hatua mtambuka ambazo zitahusisha progamu za vijana, wanawake na hata kuhusisha Balozi mbalimbali za Afrika katika suala zima la mabadiliko ya hali ya hewa na pia kuhusisha Jumuiya ya Kimataifa na kufuatilia mapendekezo mbalimbali.

Rais ameziasa Nchi za Afrika kuwa na utashi wa kisiasa na lengo la pamoja katika kukabiliana na suala hili ili kufanikisha lengo la dunia la hali ya hewa katika kipindi cha nusu ya pili ya karne ijayo. Rais amesema, ili kufanikisha juhudi mbalimbali, Bara la Afrika linahitaji msaada mkubwa wa fedha na teknolojia ya kisasa.

Mapema katika kikao cha Kamati ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa ambacho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Bwawa Ban Ki Moon, Rais Kikwete amesema mkutano ujao wa UN kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani ni chachu ya makubaliano ya Mkataba wa Hali ya Hewa ifikapo 2015.

Ripoti za karibuni kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa inaonesha kuwa hali ya Kilimo, Afya, Maji na Nishati ziko hatarini na kwamba joto duniani limepanda kwa sentigredi 0.85, hali ambayo inaashiria hali mbaya. Mkutano wa Viongozi wa Afrika (AU) umekamilika tarehe 27 jioni na Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani tarehe 28 Juni, 2014.