DKT. ABDALLAH OMARI KIGODA (MB.), WAZIRI WA VIWANDANA BIASHARA AONGOZA MKUTANO WA 99 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA AFRIKA, CARIBEAN NA PASIFIC NA MKUTANO WA 39 WA PAMOJA KATI YA ACP NA EU JIJINI NAIROBI KENYA HIVI KARIBUNI.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi. Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na Ulaya katika ukumbi wa Kenyata International Convention Centre hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya. Kushoto kwa Rais Kenyata ni Rais wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Kyriakos Gerentopoulos. Ujumbe wa Tanzania ulishirikisha pia Janet Mbene (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara (aliyevaa gauni la kijani).
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), na Rais wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika, Carribean na Pacific akiongoza Mkutano wa 99 wa Baraza hilo la Mawaziri. Kushoto kwake ni Adan Abdulla Mohamed, Waziri wa Viwanda wa Jamhuri ya Kenya akifuatilia mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre, Nairobi Kenya.
Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara akimshukuru Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na Ulaya katika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre jijini Nairobi, Kenya.