Filamu ya Espinho da Rosa Yatwaa Tuzo Nne

Malkia wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose) ya Filipe Henriques kutoka Guinea Bissau ADY de Batista akiwasili huku akiongozana na Meneja wake Sholey Maqueta kwenye usiku maalum wa tuzo wakati wa tamasha la 17 la ZIFF 2014 lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar kwenye viunga vya Ngome Kongwe.(Picha

Malkia wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose) ya Filipe Henriques kutoka Guinea Bissau ADY de Batista akiwasili huku akiongozana na Meneja wake Sholey Maqueta kwenye usiku maalum wa tuzo wakati wa tamasha la 17 la ZIFF 2014 lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar kwenye viunga vya Ngome Kongwe.(Picha

 

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

FILAMU ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose) ya Filipe Henriques kutoka Guinea Bissau imeondoka na tuzo tatu katika tamasha la 17 la filamu la kimataifa la Zanzibar (ZIFF).

Tuzo hizo ni pamoja na ya Signis , tuzo ya majaji na tuzo ya fedha ya ZIFF.

Katika tamasha hilo filamu iliyotwaa tuzo ya dhahabu ni ile ambayo ilikataliwa kuoneshwa nchini Nigeria ilikotengenezwa ya Half of a Yellow Sun iliyoongozwa na Biyi Bandele.

Shughuli za utoaji tuzo ambazo zilitanguliwa na hotuba ya makamu mwenyekiti wa kampuni ya wananchi Group ambayo brand yake ya zuku ndio inafadhili ZIFF pamoja na tuzo zake za Swahili, zilinogezshwa na vikundi mbalimnbali kikiwemo cha kereografu cha B 6.

Aidha mwenyekiti huyo alisema kwamba Zuku itaendelea kuhakikisha inasaidia kuinua kiwango cha uigizaji na utengenezaji sinema za Kiswahili kwa kutambua kwamba filamu hizo ni sehemu ya uzalishaji wa fedha katika taifa kupitia utamaduni.

Aidha alisema pamoja na mamilioni ya shilingi walioyoahidi kutumbukiza katika miaka 10 ni vyema taasisi nyingine hasa za umma kutambua uwapo wa tamasha hilo ambalo likitumika vyema ni chanzo kikuu cha fedha kwa serikali na watu wake.

Katika utoaji wa tuzo ambao ulionekana nchi ya Afrika Kusini kufanya vyema, mtendaji wa ZIFF Professor Martin Mhando alizungumza maana ya nchi za majahazi na nini kinastahili kufanywa. Chanzo  MOblog.

DSC_1071

Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akiwakaribisha wageni waalikwa waliohudhuria usiku maalum wa tuzo za tamasha la 17 la ZIFF 2014 zilizofanyika mwishoni mwa juma.

Alisema tamasha hilo halitabadili wajibu wake wa tangu awali wa,mkuchochea mabadiliko miongoni mwa jamii na serikali hali ambayo inajenga jamii yenye kuheshimu maendeleo na wajibu wa kila mmojawao.

Alisema pamoja na kuwa na safari ndefu bado ZIFF ndio jukwaa lenye uhakika kwa watengeneza sinemakatika bara la Afrika na kadhalika.

Katika utoaji tuzo,ZIFF ilialika zaidi ya watengeneza filamu 30 kutoka nchi mbalimbali.

ZIFF 2014 – AWARDS

SIGNIS AWARDS

SPECIAL MENTION

Shadow Tree

By BIja Viswa

(Tanzania)

EAST AFRICAN TALENT AWARD (1000 dollars)

Sticking Ribbons

by Bill Jones

(Kenya)

SIGNIS PRIZE

Espinho Da Rosa/ The Thorn Of The Rose

by Filipe Henriques

(Guine Bissao)

SEMBENE OUSMANE AWARDS

Umunthu,

by Mwizalero Nyirenda

(Malawi)

Body Games,

by Richard Pakleppa& Matthias Rohrig Assuncao

(Namibia / Brasil / South Africa)

SPECIAL MENTION

Welcome to Loliondo

by Morten West

(Denmark)

ZUKU BONGO MOVIES AWARDS

ZUKU PEOPLE CHOICE

Shikamoo Mzee

DSC_1085

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Bw. Richard Bell akizungumza na wageni waalikwa wakati utoaji tuzo za ZIFF 2014 lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar. Aidha mwenyekiti huyo alisema kwamba Zuku itaendelea kuhakikisha inasaidia kuinua kiwango cha uigizaji na utengenezaji sinema za Kiswahili kwa kutambua kwamba filamu hizo ni sehemu ya uzalishaji wa fedha katika taifa kupitia utamaduni na kutoa wito kwa wasanii wa Bongo Movie kupeleka kazi zao kwa ajili ya kuonyeshwa kwenye chaneli za ving’amuzi vya ZUKU na kujitangaza kimataifa kupitia ving’amuzi hivyo.

BEST ACTOR

Jackson Kabirigi

for Kisate and Nguvu ya Imani

BEST ACTRESS

Esha Buheti

for Mimi na Mungu wangu

BEST DIRECTOR

Issa Musa Cloud

for Shahada

BEST FEATURE FILM

Shahada

Issa Musa

ZIFF AWARDS

LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD

Emerson Skeens

Founder of ZIFF

Awarded Posthumously

BEST DOCUMENTARY

Sobukwe: A Great Soul

Mickey Madoda Dube

(South Africa)

BEST ANIMATION

Khumba

Anthony Silverston

(SouthAfrica)

BEST SHORT FILM

Shadowtree

Mti Wakivuli / Biju Viswanath

(India / Tanzania)

BEST EAST AFRICAN TALENT

The King’s Virgin

Daniel Moss

(Tanzania/UK)

DSC_1118

Mmoja wa majaji wa tuzo za Signs kwenye tamasha la ZIFF 2014, Adinda Pamela akitangaza washindi wa tuzo hizo. Katikati ni Mratibu wa Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na kulia ni mmoja wa “ushers” akiwa ameshikilia tuzo hiyo.

CHAIRMAN’s AWARD

Sodiq

Adeyemi Michael

(UK)

SPECIAL JURY AWARD

Julio Mesquith

Main Actor

The Thorn of the Rose

BEST FEATURE FILM (SILVER DHOW)

The Thorn of the Rose – Espinho da Rosa

by Filipe Henriques (Guinea Bissau)

BEST FEATURE FILM (GOLDEN DHOW)

Half of a Yellow Sun

Biyi Bandele (USA)

DSC_1159

Mmoja wa washindi wa tuzo za Signis alikuwa ni ADY de Batista malkia wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose). Pichani ni ADY de Batista akisindikizwa jukwaani kupokea tuzo na Meneja wake.

DSC_1160

Mmoja wa majaji wa tuzo za Signis Adinda Pamela akimpongeza ADY de Batista baada ya kunyakua tuzo hizo.

DSC_1171

ADY de Batista akiongea kwa furaha kwenye usiku maalum wa tuzo za Signis katika kusheherekea tamasha la 17 la ZIFF lililomalizika mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar.

DSC_1175

DSC_1202

ADY de Batista akishuka jukwaani baada ya kupokea tuzo na Meneja wake.

DSC_1221

Channel Coordinator wa ZUKU Swahili, Bilha Olimba akitangaza jina la mshindi wa tuzo za ZUKU PEOPLE’s CHOICE. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell

DSC_1223

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford akielekea jukwaani kumchukulia msanii mwezake Jacob Steven almaarufu kama JB alitwaa tuzo ya ZUKU PEOPLE’S CHOICE kupitia filamu yake ya SHIKAMOO MZEE kwenye tamasha la 17 la ZIFF lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar.

DSC_1231

Shamsa Ford akizungumza kwa niaba ya JB kabla ya kupokea tuzo hiyo.

DSC_1241

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell akikabidhi tuzo ya ZUKU PEOPLE’s CHOICE kupitia filamu ya SHIKAMOO MZEE ya mwigizaji Jacob Steven almaarufu kama JB iliyopokelewa na msanii mwenzake Shamsa Ford.

DSC_1245

Shamsa Ford akishukaa jukwaa kwa furaha isiyona kifani.

DSC_1267

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell akimkabidhi tuzo mwigizaji bora Jackson Laurent Kabirigi kupitia filamu ya Kisate na Nguvu ya Imani” (wa pili kushoto) aliyeambatana na ndugu yake Feysal Arikardy (kushoto).

DSC_1283

Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, William Mtitu akielekea jukwaani kumpokelea tuzo mwongozaji wa filamu Issa Mussa a.k.a Cloud 112 aliyetwaa tuzo ya uongozaji bora kupitia filamu yake ya SHAHADA ndani ya tamasha la 17 la ZIFF 2014.

DSC_1285

Kwa picha zaidi ingia hapa