Maadhimisho ya Ekaristi Takatifu Yaangusha Mapepo Tabata

Maandamano ya maadhimisho ya Ekaristi Takatifu yaliyofanyika leo katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata jijini Dar es Salaam yakiendelea kwa waumini kuzunguka katika maeneo anuai yaliyopangwa.

Maadhimisho ya ekaristi takatifu yakiendelea kama ilivyopangwa ambapo waumini walizunguka na ekaristi takatifu katika vituo kadhaa mitaa ya Tabata huku waamini kwa pamoja katika maandamano wakimtangaza Kristu kupitia ekaristi takatifu.

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha maombi cha Karismatiki kilichopo ndani ya Kanisa Katoliki, wakishusha maombi kutuliza mapepo hayo na kuyaamuru yatoke.

Mwanamke huyo akiwa ametulia (aliyelala) baadhi ya wanachama wa kikundi cha maombi cha Karismatiki Katoliki, kumuombea na kutulia.

Mwanamke huyo akiwa ametulia (aliyelala) baadhi ya wanachama wa kikundi cha maombi cha Karismatiki Katoliki, kumuombea na kutulia.

Maandamano ya maadhimisho ya Ekaristi Takatifu yaliyofanyika leo katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata jijini Dar es Salaam yakiendelea kwa waumini kuzunguka katika maeneo anuai yaliyopangwa.

Maandamano ya maadhimisho ya Ekaristi Takatifu yaliyofanyika leo katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata jijini Dar es Salaam yakiendelea kwa waumini kuzunguka katika maeneo anuai yaliyopangwa.

Wanachama wa moyo mtakatifu wa Yesu, wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya Ekaristi Takatifu yaliyofanyika leo katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata jijini Dar es Salaam yakiendelea kwa waumini kuzunguka katika maeneo anuai yaliyopangwa.

Na Mwandishi Wetu
MAADHIMISHO ya Ekaristi takatifu yaliyofanyika leo katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata jijini Dar es Salaam yameibua mapepo toka kwa muumini mmoja na kuzua tafrani huku ibada ya ekaristi ikiendelea ndani ya kanisa hilo.

Tukio hilo lilitokea leo majira ya alfajiri ambapo wakati misa ya maadhimisho ya ekaristi takatifu ikiendelea alisikika muumini mmoja akipiga kelele na kutimua mbio akitaka kumvamia padre aliyekuwa akiongoza ibada hiyo.

Baadhi ya waumini walimshika muumini huyo wa kike na kumtoa nje kwa msaada zaidi wa kumuombea ili mapepo aliyokuwa nayo ambayo yalishindwa kuhimiri nguvu za kiroho kanisani na kulazimika kukimbia huku akipiga kelele. Baada ya kutolewa nje ya kanisa huku ibada ikiendelea mwanamke huyo alianza kuombewa na kikundi cha maombi cha Karismatiki kilichopo ndani ya Kanisa Katoliki, wakikemea mapepo hayo na kuyaamuru yatoke.

“…Huyu anamapepo mabaya ambayo yalikuwa na lengo baya lakini yameshindwa kwa nguvu za kiroho, unajua leo tunaadhimisha maadhimisho ya ekaristi takatifu maadhimisho haya yananguvu za kipekee sasa watu wenye mapepo ya kichawi hawawezi kusogea lazima yawaumbue,” alisema mwana maombi mmoja aliyekuwa akimuombea mwanamama huyo.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema baada ya ibada ya ekaristi takatifu kuanza na kuvukizwa ubani mama huyo alishindwa kuvumilia hivyo kupiga mayowe huku akitimua mbio akitaka kwenda kumvamia padre aliyekuwa anaongoza ibada.
Hata hivyo kabla ya kitendo hicho alishikwa na baadhi ya waumini pamoja na wahudumu wa kanisa na kutolewa nje ambapo alianza kuzungumza alichotaka kukifanya ndani ya kanisa hilo.

Kwa mujibu wa mashuhuda walidai alisema mapepo yake yalimuamuru aende kumvamia padre ili ampige vibao jambo ambalo lilimshinda hivyo kuanza kupiga mayowe, huku akiombewa na kikundi cha wanamaombi wa Karismatiki Katoliki.
Mmoja wa waumini ambaye pia ni Mjumbe wa Tabata Msewe, eneo anapokaa mwanamke huyo, Antony Lymo alisema mwanamke huyo alipandwa na mapepo baada ya kuvukizwa ubani kwenye ekaristi takatifu hivyo kuanza kufanya fujo kabla ya kutolewa nje.

“…Unajua maadhimisho ya ekaristi takatifu yana nguvu za kiroho hivyo kama wewe ni mchawi, unamapepo mabaya ikifika eneo hilo lazima uumbuke tu na ndiyo maana mapepo yale yalimpanda,” alisema Lymo.
Hata hivyo baada ya kuombewa na kutulia mwanamke huyo ambaye ni mama wa watoto wawili alianza kusema kuwa nyumbani kwake pia ana begi ambalo lina dhana zake alizopewa na mapepo hivyo kama wanataka kumnusuru aache waende wakavichukuwe na kuviteketeza.

Maadhimisho ya ekaristi takatifu yaliendelea kama ilivyopangwa ambapo waumini walizunguka na ekaristi katika vituo kadhaa mitaa ya Tabata huku waamini kwa pamoja katika maandamano walizunguka kumtangaza Kristu kupitia ekaristi takatifu.