Pilikapilika za washindi mara baada ya kuwasili nchini kutokea Brazil kula bata baada ya ushindi kupitia kampeni ya Winda Tiketi ya Brazil na Serengeti iliyokuwa ikichezeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Lager. Kulia ni Deusdedit Kahwa kutoka Dar es Salaam, Bi Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro (katikati) pamoja na kushoto ni mwenyeji wa washindi hao Bw. Allan Chonjo Meneja Masoko wa kampuni ya Serengeti.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo akiwaongoza washindi wa tiketi ya Winda SAFARI YA Brazil na Serengeti mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere. Nyuma ni Bi Juliana Joseph Masawe (mshindi)
Bi. Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro akieleza kwa kufuraha juu ya mambo mazuri aliyoyaona nchini Brazil huku akiwashukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kumwezesha kula bata kiasi ambacho hakutegemea maishani mwake.
Menrad Faustin Shayo kutoka Arusha akihojiwa na waandishi mara baada ya kurejea nchini. Bw. Shayo alielekea nchini Brazil baada ya kushinda tiketi kupitia kampuni ya bia ya Serengeti. Shayo aliambatana na washindi wawili katika ziara ya utembelea vivutio mbalimbali.