TGNP Yafanya Mjadala wa Wazi Juu ya Uboreshaji na Uwajibikaji

Moses Iriria, kutoka ANSAF (Mtafiti) akiwasilisha mada katika mjadala huo.

Moses Iriria, kutoka ANSAF (Mtafiti) akiwasilisha mada katika mjadala huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria akiwasilisha mada wa washiriki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria akiwasilisha mada wa washiriki.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa TGNP Matandao, Bi. Usu Mallya akiendesha majadiliano kwa washiriki.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa TGNP Matandao, Bi. Usu Mallya akiendesha majadiliano kwa washiriki.

Ofisa Miradi wa TAWJA, Asha Komba ikiwasilisha mada yake katika mjadala wa wazi.

Ofisa Miradi wa TAWJA, Asha Komba ikiwasilisha mada yake katika mjadala wa wazi.

Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi.

Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi.

Sehemu ya washiriki wa mjadala huo wa wazi.

Sehemu ya washiriki wa mjadala huo wa wazi.

Pichani juu ni baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakichangia mada anuai.

Mwanaharakati Badi Darusi akiwasilisha mada yake.

Mwanaharakati Badi Darusi akiwasilisha mada yake.

Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi.

Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MTANDAO wa Jinsia nchini (TGNP Mtandao) umefanya mjadala wa wazi ulioshirikisha taasisi mbalimbali zisizo za Serikali (NGO’s) pamoja na wadau wa masuala ya kijinsia juu ya uboreshaji wa uwajibikaji kwa kuzingatia mgawanyo wa rasilimali kijinsia kwa huduma bora za kijamii nchini Tanzania.

Mjadala huo wa wazi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Blue Pearl, pamoja na mambo mengine lengo kuu ilikuwa ni kuimarisha sauti ya pamoja kudai uwajibikaji kwa watunga sera kwa kuzingatia mgawanyo wa rasilimali kijinsia, kupiga vita rushwa na kuboresha utoaji huduma za kijamii.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa mjadala huo, Kaimu Meneja wa Habari na Mawasiliano wa TGNP Mtandao, Bi. Kenny Ngomuo alisema malengo mahususi ya mjadala ni pamoja na kukuza uelewa wa muktadha wa kimataifa, kitaifa na kijamii na athari zake kwa maisha ya wanawake walioko pembezoni.

Alisema lengo lingine ni kwa washiriki kubadilishana uzoefu na mafanikio ya harakati mbalimbali kuhusu uchambuzi wa bajeti na ufuatiliaji wa utendaji katika ngazi za jamii hadi taifa na pia kuweka mikakati ya kuendeleza mapambano zidi ya rushwa, kukuza utawala bora ili kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii.

“…Malengo mengine mahususi kwa washiriki wa mjadala huu ilikuwa kuweka kumbukumbu za mafanikio yanayohusiana na mapambano dhidi ya rushwa ikiwa ni pamoja na kupigania bajeti ya kijinsia na ufuatiliaji. Kuimarisha mitandao na ujenzi wa nguvu za pamoja juu ya masuala ya bajeti ya kijinsia, vita dhidi ya rushwa na huduma bora kwa jamii,” alisema Bi. Ngomuo.

Kabla ya kuanza kwa mjadala huo mada mbalimbali ziliwasilishwa kwa washiriki, ambazo ziligusa maeneo anuai ya huduma za kijamii, rushwa na changamoto nyingine zinazoikabili jamii kabla ya wajumbe kupata fursa ya kujadiliana kwa pamoja. Takribani washiriki 130 kutoka Dar es Salaam na mikoa ya jirani ikiwemo Morogoro na Pwani wameshiriki mjadala huo.