Daladala Dar Zagoma Kwenda Mwenge…!

Daladala zikiwa zimeegeshwa baada ya kugoma kuendelea na safari kuelekea Mwenge.

Daladala zikiwa zimeegeshwa baada ya kugoma kuendelea na safari kuelekea Mwenge.

Baadhi ya madereva na makondakta wakilikimbiza basi la UDA ambalo lilimjeruhi mkononi mmoja wa madereva hao wakati akijaribu kulizuia basi hilo lisitoke ndani ya kituo cha Makumbusho kuendelea na safari kuelekea Mwenge.

Mkaguzi kutoka Sumatra akiongea na Vyombo vya habari na madereva na makondakta.

Mkaguzi kutoka Sumatra akiongea na Vyombo vya habari na madereva na makondakta.

Madereva na Makondakta wakizuia magari mengine kupita na kupeleka abiria.

Madereva na Makondakta wakizuia magari mengine kupita na kupeleka abiria.

ABIRIA wanaotumia njia ya Makumbusho kuelekea Mwenge kutokea Tandika, Buguruni na Mbagala leo wameonja joto ya jiwe kwa takribani masaa kadhaa baada ya mabasi yanayotumia kituo cha ndani ya Makumbusho kugoma kupeleka abiria Mwenge kutokana na ubovu wa barabara za ndani wanazotumia kupita kwenda Mwenge.

Sakata hilo lilianza majira ya mchana pale magari yalipofika kituo cha ndani cha Makumbusho na kuwashusha abiria wote na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea Mwenge, wakigomea ubovu wa barabara wanayotumia.

Hali hiyo ilizua mzozo mkubwa jambo lililosababisha Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra) na vyombo vya Usalama kufika eneo la tukio na kufanya mazungumzo na madereva pamoja na makondakta hao, lakini wahusika waliendelea kugoma mpaka pale walipoahidiwa kuwa ndani ya wiki moja barabara hizo zitakuwa zimerekebishwa na kuwa nzuri hivyo kwa sasa watumie barabara kuu kuelekea Mwenge.