Uganda Yaongoza Vita Dhidi ya Utapiamlo

Utapiamlo Uganda 
Na Ronald Ndungi, EANA, Arusha

UGANDA inaongoza katika vita dhidi ya utapiamlo sugu na kuudhibiti miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa mujibu wa Shirika la Umoja Mataifa Linaloshughulikia Watoto (UNICEF).
 
Mkuu wa Lishe wa UNICEF nchini Kenya, Grainne Moloney aliwaambia waandishi wa habari jijini Nairobi mwishoni mwa wiki kwamba Uganda ni nchi pekee ya EAC iliyofanikiwa kufikia wastani wa mwaka wa kupunguza utapiamlo sugu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa zaidi ya asilimia mbili tangu mwaka 2000.
 
“Tunaziomba serikali kuongeza kiasi cha bajeti kinachotengwa kwa ajili miradi maalumu ya lishe,” alisema Moloney wakati wa kuzindua Taasisi ya Kirai ya Kupambana na Utapiamlo (SUN).
 
SUN ni taasisi ya dunia inayofanyakazi ya kuimarisha vita dhidi ya utapiamlo na kufikia mwaka 2014 idadi ya nchi ambazo ni wanachama wa taasisi hiyo imefikia 50. Nchi zote wanachama wa EAC zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi ni mwanachama.
 
SUN ilianzishwa kwa misingi ya ukweli kwamba watu wote wana haki ya kupata chakula na lishe bora.
Moloney alisema tasisi hiyo inaleta pamoja serikali, asasi za kiraia, UN, wafadhili, wafanyabiashara na watafiti ili kushirikina katika kuboresha lishe katika jamii.
 
Wakati Tanzania ina idadi ya watoto wanaokadiriwa kufukia milioni 3.3 wanaokabiliwa na utapiamlo, ina milioni 2.8 na Uganda milioni 2.3. Katika hilo Burundi ina jumla ya watoto wenye utampialo sugu 809,000 wakati Rwanda ianao watoto 684,000.