Mashujaa Bendi Kufanya Ziara Mikoani

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa Maximillian Luhanga (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari jana kuhusu ziara yao itakayofanyika katika mikoa yote baada ya mfungo wa Mwezi wa Ramadhan, kustoto ni rapa wa bendi hiyo Raja Ladha (Na Mpiga Picha Wetu)

Na Mwandishi Wetu
 
BENDI ya muziki wa dansi nchini Mashujaa, inatarajia kufanya ziara katika mikoa ya nchini nzima kwa ajili ya kutoa shukrani kwa mashabiki wao waliowapigia kura kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Awards.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi hiyo Maximillian Luhanga, alisema kuwa wamepata mafanikio makubwa kwa miaka miwili baada ya kupata tuzo nane. Alisema kuwa mwaka jana walipata tuzo tano na mwaka huu wamefanikiwa kupata tuzo tatu kutokana na kura za mashabiki wao. Alisema kuwa wamejifunza mambo mengi katika muziki kutokana na kuwa wanakubali ushauri kutoka kwa mashabiki wao.
 
“Tunatarajia kufanya ziara katika mikoa yote ya Tanzania baada ya kupata tuzo tatu mwaka huu na hivyo hiyo ziara itakuwa kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki wetu,” alisema.
 
Alisema kuwa wamesharekodi nyimbo mbili mpya ambazo watazitumia mikoani ikiwa ni kama zawadi kwa mashabiki wao, ambapo nyimbo hizo ni Usidharau Sifuri na Kiu ya Haki. Alisema kuwa ili waendelee kuwa karibu na mashabiki wao kila mwezi watakuwa wanatengeneza matukio mbalimbali ya bendi katika mitandao ya Kijamii.